Umoja wa wazazi CCM mkoa Shinyanga umetoa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kutokana na kutekeleza ipasavyo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutetea haki za wanyonge pamoja na kuiletea nchi mafanikio makubwa ya kimaendeleo.
Tamko la umoja huo wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, limetolewa leo Agosti 14, 2019 kwenye kongamano la umoja huo, ambao limehudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya ya Kishapu, Kahama, Shinyanga vijijini, na manispaa ya Shinyanga, ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa, huku mgeni rasmi akiwa mjumbe wa NEC Gaspar Kileo.
Akisoma tamko hilo, Katibu wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, amesema wanampongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ipasavyo, ambapo ndani ya miaka minne tangu alipoingia madarakani amefanya mambo makubwa ikiwamo kuiletea nchi maendeleo.
“Sisi Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga tunatoa tamko la kupongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100, ambapo ndani ya miaka yake minne tu akiwa madarakani amefanya mambo makubwa sana katika nchi yetu, hivyo lazima tumpongeze na kumuombea pia,”amesema Salu.
“Mambo ambayo ameyafanya Rais wetu na anapaswa kupongezwa ni pamoja na kudhibiti mafisadi, rushwa, mishahara hewa, utoroshwaji wa makinikia, upotevu wa mapato, kaboresha mikataba mibovu ya madini, elimu bure, ujenzi wa madaraja, miundombinu ya barabara, reli ,huduma za afya, ununuaji wa ndege, na makazi ya watumishi,”amefafanua Salu.
Naye mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la kumpongeza Rais John Magufuli mjumbe wa halmashauri kuu Taifa mkoani Shinyanga (NEC) Gaspar Kileo, akipokea tamko la pongezi hizo kwa niaba ya Rais Magufuli, ameupongeza umoja huo wa wazazi CCM mkoani humo kwa kutambua kazi kubwa ambayo anaifanya rais Magufuli.
Amesema mbali na pongezi hizo, lakini zawadi pekee ambayo wanapaswa kumpa Rais John Magufuli, ni kumpatia ushindi wa kishindo kwa asilimia 100 kwenye changuzi zote kuanzia serikali za mitaa mwaka huu, pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020,wapinzani wasiweze kupata hata kiti kimoja cha ushindi waambulie zero.
Aidha amesema ushindi huo ndiyo itakuwa zawadi kubwa kwa Rais John Magufuli ikisindikiza tamko lao la pongezi, huku akiwataka pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, na kuhamasisha majirani zao, ndugu, jamaa na marafiki, ili waweze kupiga kura na kuipatia ushindi huo mnono CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Salum Abdalah Simba akizungumza wakati Umoja huo ukitoa tamko la kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kikamilifu ilani ya CCM.
Katibu wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu akisoma Tamko la umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uchapakazi wake wa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100.
Katibu wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, mkono wa kulia akimkabidhi tamko la kumpongeza Rais John Magufuli, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC mkoani Shinyanga Gaspar Kileo kwa niaba ya Rais ambapo atamfikishia tamko lao.
Kitabu chenye tamko la Umoja wa Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mjumbe wa halmashauri kuu taifa (NEC) Gaspar Kileo akiteta jambo na mwenyekiti wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba,kwenye kongamano la kupongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100.
Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo, akizungumza mara baada ya kupokea Tamko la umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia 100 ndani ya miaka minne tu.
Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo, akiwa asa wajumbe wa umoja huo wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kuwa licha ya pongezi hizo, bali wanatakiwa wampatie zawadi Rais John Magufuli ya ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zote kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.
Mchungaji Elias Madoshi kutoka kanisa la FPCT Shinyanga akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Shekhe Alhaji Ibrahimu Ramadhani akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Wajumbe wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani.
Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.
Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani.
Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.
Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM.
Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.
Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM.
Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.
Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha na MNEC Gaspar Kileo mara baada ya kupokea tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli.
wajumbe wakiendelea kupiga picha.
Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiserebuka huku wakibeba tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli.
Wajumbe wakendelea kuserebuka.Awali mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo mkono wa kulia akiingia ukumbini kwenye Kongamano la umoja wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli, kushoto ni mwenyekiti wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba.
Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo akiwasili kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupokea Tamko la kumpongeza Rais John Magufuli lililoandaliwa na umoja wa wazazi CCM Mkoani humo, ambapo amepokelewa na viongozi wa umoja huo, huku akiwa ameshikana mkono na katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu.
Askofu Josephat Musira wa kanisa la TMRC- Ndembezi Shinyanga mjini, akimwombea Rais John Magufuli, pamoja na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, na waziri mkuu Kassim Majaliwa na wateule wake wote wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, Mungu awajalie afya njema na kuendelea kuchapa kazi ya kutumikia wananchi na kuleta maendeleo ya taifa.