Homa ya Mapambano ya Ubingwa Afrika Mashariki na kati imezidi kupanda baada ya Timu teule ya Mieleka ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania iliyoteuliwa kushiriki mashindano ya majeshi ya Dunia mwezi Oktoba kushiriki kuonyesha uwezo wao Agost Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kocha wa Timu hiyo teule ya JWTZ ya Mieleka Sajini Boniventura Kamugisha alisema kibali kimetolewa kwa Timu hiyo kwa mara ya Kwanza kupanda Katika Jukwaa La Mapambano ya kulipwa lakini wao wakiwa wanajiandaa na Mashindano makubwa Duniani.
Aliwataja wachezaji watakaocheza 10 wataoyeshana Ubabe ambao ni Eliudi Mganga, Burhan Abdalah , Abraham Nkabuka, Jumanne Mteleka , Emanuel Kamwela , Cheyo Malugu, Aron Kaila, Joseph Kakiziba, Subiri Newton, Ally Basha.
” Kinachokuja kuonyeshwa ni umahiri wa timu ili kutoa hamasa kwa watanzania ili kuwaobyesha na kuwatia nguvu katika Mashindano ya Dunia kwa hiyo Wanachi waje washuhudie Timu yao siku hiyo ya Tarehe 24 Agosti Club 361 Lugalo Mwenge ” Alisema Kamugisha.
Kocha wa Timu hiyo teule Aliongeza Mashindano hayo wanayachukulia kwa Uzito mkubwa kwani Licha ya Kuwakilisha Jeshi lakini Wanawakilisha Nchi.
Kwa upande wake Mratibu wa kiufundi wa pambano hilo Yassin Abdalah amesema uwepo wa mdhamini Smartgin ni hatua kubwa muhimu inayopelekea kufufua aria ya mchezo huo na kuondokana na Ubabaishaji wa Maslahi ya Mabondia.
” Club 361 kwa kushirikiana na peaktime ni waandaaji mahiri wenye uaminifu hivyo smartgin wameingia sehemu sahihi na tunawaunga mkono sambamba na kuwakaribisha wadhamini wengine” Alisema Ustaadh.
Aliongeza kuwa katika Masuala yote ya Kiufundi yanaenda vizuri ikiwemo afya za mabondia na wanaendelea na mazoezi kwama walivyopangiwa na walimu wao.
Aliwataja Mabondia wanaowania mkanda wa Afrika Masharuki na Kati kuwa ni Nasibu Ramadhani na Issa Nampepeche wakati Haidary Mchanjo na Tonny Rashidi na katika Mapambano ya Utangulizi Lukmani Ramadhani vs Ismail Haridi Bakari Dunda na Kudura Tamimu wataonyeshana kazi.
Naye Mratibu Mkuu wa Pambano hilo Selemani Semunyu alisema licha ya kuwepo kwa mapambano hayo pia kutakuwa na Mapambano ya Mabondia kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaojiandaa na Mashindano ya Dunia ya Majeshi Nchini China.
Semunyu alisema Mabondia hao wataongozwa na Koplo Selemani Kidunda ambaye atapigana na Bondia Nassoro Hussein lengo likiwa ni kujipima kuelekea Mashindano hao na kutia hamasa kwa Wananchi na Mabondia
Pambano hilo la Ngumi linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 Mwezi huu limeandaliwa na Club 361 kwa kushirikiana na PeakTime na Solid Rock na kudhaminiwa na Smart Gin, Kiwango Security na Resolution Insurance.