NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
KITUO kipya cha afya Kerege ,Bagamoyo, mkoani Pwani ,kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme mbadala hali inayosababisha hofu endapo itatokea umeme kukatika ghafla huku upasuaji mkubwa ukiwa unafanyika.
Kutokana na hali hiyo ,kunahitajika genereta ama solar ambalo litasaidia wakati itatokea dharula ya kukatika umeme.
Aidha ,kituo hicho kinakabiliwa pia na changamoto nyingine ya upungufu wa watumishi 19,kuongeza jengo la mama na mtoto,exray,uzio, na nyumba za watumishi.
Akitoa taarifa kwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo, alhaj Shukuru Kawambwa, wakati alipotembelea kituo hicho na kuzungumza na watumishi na wananchi katika ziara yake ya jimbo, kaimu mganga mfawidhi dkt.Asha Chanyeliela alisema, kwasasa wameshaanza kutoa huduma za upasuaji na kinalenga kuhudumia watu 8,921,tangu kituo kianze wazazi 400 wamejifungua kati yao 32 wamefanyiwa upasuaji.
Alieleza, wanashirikiana na shirika la umeme Tanesco ,wakati ikitokea umeme kukatika huku wakifanya upasuaji na wanashukuru haijawahi kutokea madhara ikitokea dharura ya aina hiyo.
“Umeme wa dharura utatusaidia,tupate genereta ama solar maana hadi sasa haijawahi kutokea madhara ,wakati umeme ukitokea na wakati huo huo ukifanyika upasuaji ,ila bora ya kinga kabla ya madhara”
Akizungumzia kuhusu watumishi ,Asha alisema ,wapo 20 mahitaji 39 na pungufu ni watumishi 19 ili kukidhi mahitaji.
Nae ,alhaj Kawambwa alisema, ujenzi wa kituo cha afya kerege ulianza tarehe 20/10/2017 na lengo kuu la mradi likiwa ni kuboresha vituo vya afya nchini na kuwa na vituo vya afya vyenye ufanisi.
Alipokea changamoto zilizotolewa na kuahidi kuzifikisha katika eneo mamlaka husika, na kubeba tatizo la upungufu wa watumishi ili waweze kuongezewa wataalamu wa afya sio tu Kerege lakini na katika vituo vya afya vingine na zahanati za Bagamoyo.
Awali diwani wa kata ya Kerege ,Saidi Ngatipura alimshukuru mbunge huyo kwa kupigania na kushiriki kusogezewa huduma za afya katika kata hiyo ambapo kwa sasa imekuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi.
Katika kata hiyo, mbunge huyo alifanya mikutano ya hadhara na wananchi eno la Kitonga,Manofu,Matumbi na kwa Kiwete