Home Mchanganyiko UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MTO RUFIJI NI MFANO KWA NCHI...

UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MTO RUFIJI NI MFANO KWA NCHI ZA SADC NA EAC, RAIS DK. MAGUFULI APONGEZWA

0

  Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa SADC, Mapolao Mokoena Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam leo.

Bw. Calicious Tutalife Mkurugenzi wa Viwanda, Maendeleo na Biashara SADC akizungumza namna jumuiya hiyo ilivyojipanga kuhusu maendeleo ya viwanda na biashara katika nchi wanachama.

Kutoka kulia ni Bw. Calicious Tutalife Mkurugenzi wa Viwanda, Maendeleo na Biashara SADC Mkuu wa Mwasiliano na Uhusiano SADC Barbara Lopi na Geofrey Tengenezwa mmoja wa wanakamati wa mkutano wa SADC.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia uwasilishaji wa mada katika mkutano huo.

Kutoka kulia ni Bw. Calicious Tutalife Mkurugenzi wa Viwanda, Maendeleo na Biashara SADC Mkuu wa Mwasiliano na Uhusiano SADC Barbara Lopi wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari.

Kutoka kulia ni Bw. Calicious Tutalife Mkurugenzi wa Viwanda, Maendeleo na Biashara SADC Mkuu wa Mwasiliano na Uhusiano SADC Barbara Lopi na Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa SADC, Mapolao Mokoena.

Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa muhimu katika mkutano huo.

……………………………………………….

Ujenzi wa mradi  wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia.

Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa SADC, Mapolao Mokoena amesema mradi huo mkubwa unaojengwa nchini ni wa kipekee, ambao unasimamiwa moja kwa moja na Serikali na unagharamiwa na fedha za ndani.

“Mradi huu mkubwa wa Rufiji ni jambo la kujivunia, sisi SADC tunajivunia na si kwa SADC tu, lakini pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ni mradi wa mfano pale utakapokamilika,” amesema.

Mokoena amempongeza Rais wa Jahuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo kubwa wa umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi za SADC huku akisema SADC inamuunga mkono katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa umeme.

Amesema mradi huo unaonesha unatoa funzo kwamba uongozi unahusika katika kuhakikisha miradi yenye tija inasimamiwa kwa nguvu zote ili kuzinasua nchi zetu katika matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa uwezo wa ndani.

Mokoena amesema kutokana na uhaba wa nishati unaozikabili nchi nyingi wanachama wa SADC, juhudi za ziada zinahitajika kuboresha upatikanaji wa nishati, ambayo ni muhimu katika kutimiza malengo ya uwekzaji katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa.

Amesema miongoni mwa mikakati muhimu ya SADC kwa sasa ni kuhakikisha kuwa na uhakika wa nishati rahisi, yenye uhakika, gharama ya chini, kupitia mpango maalumu uliowekewa ukomo wa mwaka 2027.