Home Biashara TBL ilivyoshiriki maonyesho viwanda ya SADC, Chapa ya kinywaji cha Konyagi yavutia...

TBL ilivyoshiriki maonyesho viwanda ya SADC, Chapa ya kinywaji cha Konyagi yavutia wengi

0
Maonyesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) yalifanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni ya TBL Group, chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBev, ilishiriki kikamilifu , banda lake  lilitembelewa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar, Mh.Ali Mohamed Shein na wageni wengine maarufu.

 Chapa ya kinywaji cha Konyagi ambacho kinatengenezwa na kampuni ya TDL chini ya  kampuni ya TBL Group, ilionekana kuwavutia  washiriki wengi  ikiwemo bidhaa za mvinyo na kuashiria kuwa kutokana na ubora na umaarufu wake kitaendelea kuteka masoko ya nje hususani katika nchi za SADC.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ),Mh. Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Meneja wa Mauzo ya Nje wa TDL, Maleke Hans Mringo, wakati alipotembelea  banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya viwanda ya SADC.

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwa katika banda lao la maonyesho

Baadhi ya wafanyakazi wakiwa na cheti cha udhamini ambacho Kampuni ilitunukiwaBaadhi ya wafanyakazi wakiwa na cheti cha udhamini ambacho Kampuni ilitunukiwa

Meneja mawasiliano Mwandamizi wa TBL,Amanda Walter akipokea cheti cha udhamini wa wiki ya maonyesho Viwanda kwa nimba ya Kampuni kutoka kwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai.