Home Mchanganyiko MKOA WA PWANI WADHAMIRIA KUWA UKANDA WA VIWANDA,”WAFIKIA VIWANDA 836-NDIKILO

MKOA WA PWANI WADHAMIRIA KUWA UKANDA WA VIWANDA,”WAFIKIA VIWANDA 836-NDIKILO

0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani unaendelea kujipanga na kuonyesha adhma yake ya kudhamiria kuwa ukanda wa viwanda ambapo kwa sasa una jumla ya viwanda 836 .
Kati ya viwanda hivyo vikubwa vipo 56,vya kati vipo 80 na viwanda vidogo 338 huku viwanda vidogo sana vimefikia 362.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliweka bayana hayo wakati alipokuwa akielezea kuhusiana na namna wavyoshirikiana na sekta binafsi katika shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali.
Hata hivyo alieleza, pia halmashauri zimetenga maeneo kwa ajili ya viwanda hekta 22,937 ,hivyo amewataka wawekezaji kukimbilia fursa hiyo.
“Ila zipo changamoto za fidia na upimaji wa maeneo husika,licha ya jitihada kufanywa na halmashauri kuuza maeneo kwa bei kubwa na kutenga fedha za ndani ili kufidia gharama za upimaji na fidia,”
Ndikilo alisema ,serikali inaendelea kufuta hati za watu wasioendeleza maeneo yao na kuyaacha pori na kuyapangia matumizi mbalimbali ikiwemo shughuli za viwanda na uwekezaji,”:Halmashauri endapo zitabaini mashamba na maeneo yasiyoendelezwa wanapendekeza yanatwaliwa na serikali kwa ajili ya uzalishaji,uwekezaji na kilimo.
Aliwaomba wafanyabiashara na wawekezaji kukimbilia mkoani Pwani kwenda kujenga viwanda kwani maeneo yapo ya kujenga viwanda vikubwa,vya kati na hata vidogo.
Katika hatua nyingine, mkoa huo unashirikiana na sekta binafsi kuboresha mazingira ya kibiashara na uwekezaji,kuwaweka katika umoja wafanyabiashara kwa kuanzisha wiki ya viwanda na maonyesho na kupata fursa ya kujitangaza na kupanua wigo wa kimasoko.
Ndikilo”Mwaka 2018 tulifanikiwa kuandaa wiki ya viwanda na maonyesho hivyo tunatarajia kufanya zaidi ya mwaka uliopita ,tunaandaa kongamano kubwa la uwekezaji ili kuwaweka karibu wadau wa uwekezaji na wafanyabiashara,taasisi za fedha,taasisi za uwezeshaji ,mabalozi na wanahabari wa ndani na nje ya nchi.