Mkuu Wa Mkoa Wamorogoro Dk Kebwe Steven Kebwe na Mbunge wa
jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz Abood wakiwajualia hali baaadhi ya manusra
wa ajari ya lori lililoteketea kwa moto leo agosti 10 2019 majira ya saa asubuhi
***************
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
Kamanda wa Oparesheni na Mafunzo ya jeshi la polisiLebaratus Sabas, amesema
idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyoanguka nakupelekea kulipuka kwa
moto leo Agosti 10, imefikia 64,ambapo kati yao wanaume ni 58 na wanne ni
wanawake ambapo mmoja katika wanawake hao ni mtoto.
Kwa upande wa idadi ya majeruhi imefikia 66, wanawake wakiwa 8,ambapo kati
yao mmoja ni mtoto na wanaume 58 ambapo wote wanaendelea kupatiwa
matibabu katika Hosptali ya rufaa ya Morogoro.
Ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi katika eneo la Msamvu Mkoani Morogoro
na hadi sasa Jeshi la polisi, limekwishakamata lita takribani 206 za mafuta ya
petroli , zilizokuwa zimefichwa katika mabanda pembezoni mwa eneo la ajali
ilipotokea.
Aidha Kamishina Sabas amewataka wananchi wanaoishi kandokando ya barabara
kutokuwa na tamaa na kujiepusha na ajali ambazo zinaepukika, pamoja na
kuwataka wale wote waliopata majeraha madogomadogo na kutokomea wasisite
kwenda hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge ajira na watu
wenye uremavu Mh Jenista Muhagama amewataka watanzania kuwa wapole
katika msiba huu mzito uliowakuta.
Aidha amesema kuwa tayari serikali ameshaandaa mikakati ya kuhakikisha
majeruhi wote wanapata tiba stahiki kwa wakati,ambapo awameanda herkopta
za zarula kwa watakao hitaji tiba nje ya mkoa wa morogoro .
Hata hivyo amesema kuwa serikali imepaleka madaktari bingwa kutoka hospitari
ya taifa ya muhimbili na benjameni mkapa ya dodoma kwa ajiri ya kuwapatia
matibabu.
Aidha Kufuatia ajari hiyo Rais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania Mh Dk Jonh
Pombe Magufuri na viongozi mbalimbali wametuma salamu za pole kwa mkuu
wa Mkoa Wa Morogoro Mh Kebwe Steven Kebwe na watanzania waliofikwa na
msiba huo.