*********
KWAMBA TAREHE 09.080.2019 MAJIRA YA SAA 06:06HRS ALFAJIRI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA ENEO LA MKOLANI – MSIKITINI, GARI NAMBA T.451 AES AINA YA SCANIA MARCOPOLO BUS MALI YA KAMPUNI YA ABOOOD, LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY JUMA LIKITOKEA MWANZA KWENDA DAR ES SALAAM LIKIWA NA ABIRIA 28, LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI AKIWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA 885 AVK AINA YA SANYA AITWAYE BABU ISAYA, MIAKA 28, MHAYA, MKAZI WA NYAHINGI –MKOLANI ALIYEKATIZA GHAFLA BARABARANI TOKA KUSHOTO KWENDA KULIA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
WATU WATATU AMBAO NI ABIRIA WA BUS LA KAMPUNI YA ABOOD WAMEJERUHIWA. MAJERUHI WAMEPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA WILAYA YA NYAMAGANA NA KURUHUSIWA KUENDELEA NA SAFARI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
DEREVA WA GARI AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO ZAIDI, CHANZO CHA AJILI BADO KINACHUNGUZWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA NA AKIPATIKANA NA KOSA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. SAMBAMBA NA HILO LINAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAWEZE
KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.