Home Mchanganyiko BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO MKOMBOZI KWA WAKULIMA: WAZIRI HASUNGA

BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO MKOMBOZI KWA WAKULIMA: WAZIRI HASUNGA

0

 

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu

 

WAZIRI wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko ni mkombozi kwa wakulima hapa nchini.

 

Mhe. Hasunga ameyasema hayo alipotembelea banda la bodi hiyo kwenye
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu ambako kunafanyika maonesho ya Nanenane
kitaifa ambapo wakulima wanaonesha mazao yao lakini pia maonesho hayo
yanatumika kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa kilimo.

 

“Kwa wakulima bodi hii ni mkombozi kwa wakulima kwani jukumu lake
ni kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao ya nafaka, lakini pia bodi hii
inanunua mazao ya nafaka na kuyaongezea thamani na sasa wameanzisha kiwanda
kule Arusha cha kusaga nafaka na kuuza, lakini pia Dodoma watajenga kiwanda cha
kuchakata Alizeti na nafaka na pia Mwanza watajenga kiwanda cha kuchakata
mpunga na mazao mengine hivyo bodi hii ni muhimu kisekta.” Alisema.
 

 

Mhe. Hasunga pia ameipongeza Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
kwa kutekeleza vema maelekezo ya Serikali ya kununua na kuuza Korosho.

 

“Moja ya Jukumu tulioipatia Bodi mwaka huu ni kununua na kuuza
Korosho kwa niaba ya Serikali na kazi hiyo wameifanya vizuri, wameweza kunua
Korosho yote na wanayo.” Alifafanua.

 

Alisema, Bodi kama wafanyabiashara imeweza kununua Korosho na
kuongeza thamani (Ku- process) kwa
kuziweka kwenye vifungashio vya viwango mbalimbali na ndio maana wako kwenye
maonesho ili kuzionesha na kutangaza masoko mbalimbali kwa wadau wa ndani na
nje ili waweze kutoa Oda na hii itasaidia kupanua masoko ya Korosho.
Maonesho ya Nanenane kitaifa hapa Nyakabindi Mkoani Simiyu yalizinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Agosti 1, na yatafikia Kilele Agosti 8, 2019 na yamebeba kauli mbiu isemayo “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa ukuaji w aUchumi wa Nchi.”.
 Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, akizungumza kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu ambako Maonesho ya Nanenane kitaifa yanafanyika mkoani humo.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, (kushoto), wakielimisha wakulima hawa wa Mkoani Simiyu walipotembelea banda la Bodi hiyo kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu leo Agosti 5, 2019.
 Kikosi kazi cha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, ambacho kiko kwenye banda la bodi hiyo viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu tayari kutoa elimu kwa wananchi
 Wafanyakazi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, (kushoto), wakitoa elimu kuhusu shughuli za Bodi.