Home Mchanganyiko VIKUNDI VYA UWT WILAYA YA MUFINDI VYAFIKISHA MTAJI WA MILIONI MIAMBILI KUMI...

VIKUNDI VYA UWT WILAYA YA MUFINDI VYAFIKISHA MTAJI WA MILIONI MIAMBILI KUMI NA NNE

0
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akihutubia baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo
Baadhi ya viongoziwa chama cha mapinduzi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo
 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameendelea kuitunisha
mifuko ya kimaendeleo ya wanawake wa UWT wilaya ya mufindi kwa kukuza mitaji
waliyopewa na mbunge huyo.
 
Akizungumza kwenye mkutano mkuu
wa jimbo la Mufindi kaskazini,mbunge Rose Tweve alisema kuwa vikundi vya wilaya
ya Mufindi vinajumla ya mtaji wa milioni miambili kumi na nne (200,140,000) ambazo
zinatokana na mtaji wa awali ambao mbunge huyo aliwapa.
 
Ikumbukwe kuwa mbunge Rose
Tweve aliahidi kuviwezesha vikundi vyote vya UWT mkoa wa Iringa kwa kila kata akiwa
na lengo la kuhakikisha kuwa wanawake wanajikomboa kiuchumi kupitia fedha hizo
ambazo alikuwa amewaahidi.
 
Tweve aliwaomba wanawake wa
UWT  wilaya ya Mufindi waendelee kufanya
kazi  na kutunza mtaji huo kwa kuwa ndio
mkombozi wa uchumi na amewapongeza kwa kuwa na nidhamu ya fedha ambayo wamekuwa
na hadi hapo walipo fika.
 
“Hongereni sana wakinamama na
nawaomba viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kuendelea kuwalea na kuwapa
ushirikiano wa kutosha ili wafikie malengo yawalikusudia kwa kuwa wameonyesha
nidhamu ya matumizi ya fedha” alisema Tweve
 
Awali mbunge huyo alitoa mitaji
ya shilingi laki tano kwa vikundi vya wanawake wa kila kata kama mitaji ya
kuanzia biashara zao ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa moja moja na wa wilaya
kwa ujumla.
 
Aidha Tweve amewataka Wanawake
mkoa Iringa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya kijasiliamali bila kujali
itikadi za vyama vyao ili kuleta maendeleo.
 
“Akina mama wasikate tamaa
katika kujiunga katika vikundi mbalimbali kwani hiyo inasaidia kubadilishana
mawazo katika suala la kutekeleza maendeleo yao” alisema Tweve
 
Tweve amewataka viongozi
kuhakikisha   wanawapigania wanawake
katika kupata fursa na kuvunja mfumo dume uliopo.
 
Katika hatua nyingine amewaasa
wanawake wanapowezeshwa fedha wahakikishe wanazitumia vizuri ili kufikia
malengo yao.