**************
Na gladness mushi Arusha
Watanzania pamoja na wadau wa nyama hapa nchini wameshauriwa kujiwekea utaratibu wa kula nyama ambayo imetunzwa vema kwenye ubaridi kwa masaa8-48 ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea kwa kula nyama ambatyo bado ni nyekundu.
Kwa sasa baadhi ya walaji wa nyama hupenda kula nyama ambayo ni nyekunduau yenye damu kwa kujua kuwa ndio bora kumbe nyama hiyo ina madhara makubwa sana.
Hayo yameelezwa na kaimu msajili wa bodi ya nyama nchini Bw Imani Schalwe mapema jana wakati akiongea na “FULLSHANGWE”kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji yanayoendelea kwnye viwanja vya themi jijini Arusha.
Sichalwe alisema kuwa bodi hiyo inawashaurui walaji wa nyama kuhakikisha kuwa wanatumia nyama ambayo imepata ubaridi wa kutosha ili kuepusha madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa kula nyama yenye damu.
Alifafanua kuwa kwa kula nyama hiyo mlaji anaweza kukutana na misuli lakini kama nyama itapumzishwa kwa masaa hayo basi itakuwa kwenye viwango bora ambavyo vuinatakiwa na kujaliwa na bodi hiyo.
katika hatua nyingine aliwataka wamiliki na wauzaji wa nyama kuhakikisha kuwa wanatumia teknolojia mpya ya kukata nyama na kuchana na tabia ya kukata nyama kwa kutumia magogo ambayo yana madhara kwa afya ya mlaji.
Alitaja madhara ya kutumia magogo kukatia nyama ni pamoja na baadhi ya vijiti kubaki ndani ya nyama, kupata magonjwa ya matumbo lakini pia kupata ugonjwa wa Apendix ambao unaweza kuepukika kwa kufuata taratuibu za uuzaji wa nyama.
Alimalizia kwa kuwataka wadau wa nyama kuachana na badhi ya tabia za mitaani na badala yake wahakikishe kuwa wanatumia bodi hiyo ya nyama hapa nchini kwa kufuata taratibu pamoja na elimu kwa kuwa bodi hiyo ipo kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji.