Home Mchanganyiko VETA WAENDELEZA UBUNIFU, MAMIA WAFURIKA KUONA VIBAO VYA KUFULIA NGUO NA MASHINE...

VETA WAENDELEZA UBUNIFU, MAMIA WAFURIKA KUONA VIBAO VYA KUFULIA NGUO NA MASHINE YA KUCHAKATA NYASI

0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadfi VETA, imeendelea kuja na ubunifu katika kutengeneza mashine na vifaa mbalimbakli ili kurahisisha utendaji kazi katika maisha ya kila siku katIka jamii.
VETA ambao wako kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, banda lao limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotembeela maonesho hayo ambapo, miongoni mwa vifaa vilivyobuniwa ni kibao cha kufulia nguo, ambapo wanafunzi wa VETA mjini Songea kwa kushirikiana na Ruta Kamoto kutoka Shirika la JICA. Wamebuni njian rahisi ya kufua nguo kwa kutumia kibao.
Ruta Kamoto ambaye pia ni Afisa Maendeleo Songea vijijini alisema, kibao hicho kilibuniwa na wanafunzi wa VETA Songea ili kumrahisishia mfuaji w anguo badala ya kutumia nguvu nyingi katika kufikicha nguo, kibao hicho hakihitaji mayumiazi makubwa ya nguvuy katika kufua kwani ni rahisi na hutumia mufa mfupi kufua nguo.
“Kibao hiki kina migongo midogo, unaweza kutumia sabuni ya kipande na kupaka katika nguo kama kawaida, au kuweka nguo katika machanganyiko wa maji na sabuni ya unga baada ya kukolea, unachukua nguo na kuilaza kwenye kibao na kusugua taratibubu na baada ya muda mfupi nguo itakuwa imetakata.” Alisema Ruta Kamoto.
Aidha wananchi wanaotembelea banda hilo la VETA pia wamepata fursa ya kujionea mashine ya kusaga nyasi kwa ajili ya malisho ya mifugo, kama vile Mbuzi na Ng’ombe ambapo mashine hiyo inaweza kutumia umeme au jenereta.
Mbunifu Fredrick Uliki ambaye ni Mwalimu wa ufundi mitambo VETA Morogoro, yeye alisema wao wamebuni mashine ya kukatakata malisho ya mifugo ili yaweze kuliwa kwa urahisi, “majani yakiwa makubwa makubwa huliwa kwa asilimia kama 30 lakini ukikata nyasi kuwa ndogondogo mnyama anaweza kula hadi asilimia 90 ya chakula ulichompa, pia mashine inaweza kuchakata mahindi, dagaa na mashudu ya alizeti ili kuwezesha mifugo kama ndege na kuku kula kwa urahisi” Alifafanua Bw. Uliki.
Maonesho ya Nanenane Nyakabindi yalizinduliwa rasmi Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufikia kilele Agosti 8, 2019 huku yakiwa yamebeba kaulimbiu isemayo “Kilimoi, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uc humi wa Nchi.”.Ruta Kamoto kutoka Shirika la
JICA akielezea jinsi kibao kinavyoweza kurahisisha kazi ya ufuaji nguo kwa wananachi waliotembela banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane ,kitaifa viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


 Mwananchi akijaribu yeye mwenyewe kufua kwa kutum ia kibao hicho ambapo alikiri kuwa ni rahisi mno.

 Wananchi wakipata elimu kutoka maafisa wa VETA.

 Mwanafunzi wa VETA, akielezea jinsi mashine waliyobuni inavyoweza kunyoosha matairi ya gari (Wheel balance).