Meddie Kagere akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Power Dynamos ya Zambia Fredrick Mulamba katika mechi iliyowakutanisha Simba CP dhidi ya Power Dynamo ya nchini Zambia. Simba imeibuka na ushidi wa magoli 3-1
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara akiamshaamsha mashabiki wa timu hiyo wakati wa mchezo huo uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa.
Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji akizungumza jambo wakati wa kutambulisha wachezaji wa timu hiyo leo.
Wachezaji wa timu ya Simba na Power Dynamos ya Zambia wakiingia uwanjani leo.
*****************
NA EMMANUEL MBATILO
Mshambuliaji wa klabu ya Simba Meddie Kagere amefanikiwa kung’arisha sherehe ya Simba Day baada ya kufanikiwa kuingia kambani mara tatu katika mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Power Dynamo ya Zambia.
Kagere alionekana wa moto kwani ilichukua dakika tatu tu kuipatia klabu yake goli la kuongoza ambapo guli hilo halikudumu nao wageni wakafanikiwa kurudisha goli hilo mpaka kufikia mapumziko timu zote mbili hakupatikana mbabeba.
Simba ilirudi kipindi cha pili kwa kuhitaji ushindi katika mechi hiyo hasa hamasa za wachezaji waliokuwa uwanjani mwisho yule yule wa kumuita Meddie Kagera akongeza kalamu ya magoli mawili na kufikisha magoli matatu katika mechi hiyo
Mechi hiyo ilitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo pia utambulishaji wa kikosi kipya cha Simba kikijumuisha wachezaji wapya na wale waliokuwepo msimu uliopita.
Licha ya Ushindi huo Simba walionekana kuwa imara zaidi hasa eneo la ulinzi na ushambuliaji huku Shomari Kapombe akipata nafasi ya kucheza katika mchezo huo baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Kwa upande wa mashabiki waliojitokeza kwa wingi na kujaza kabisa uwanja huo walionekana kushangilia kwa nguvu hali iliyoleta raha kwa kila mtu aliyeshuhudia pambano hilo