Afisa Mifugo Mkuu, kutoka idara ya huduma za mifugo,Bi.Joyce Daffa akiwaelimisha wanafunzi kuhusu madhara ya kichaa cha mbwa, kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu leo (5.8.2019). Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani (kulia) akipata maelezo ya mashine ya kukatia malisho ya mifugo kutoka kwa Mkufunzi wa Mafunzo ya Mifugo kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Bw. Alex Mrema (kushoto) mara baada ya kufika katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Nyakabindi-Simiyu (05.08.2019)
Mratibu wa shughuli za uzalishaji na Uzalishaji na Ukuzaji Viumbe kwenye maji kutoka Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) – Mwanza, Bw.Peter Masumbuko akiwaelimisha wadau wa uvuvi kuhusu uvuvi bora akisisitiza kutokuruhusu samaki kuzaliana kwenye mabwawa kwa kuwahasi samaki kwa ukuaji bora.Darasa hilo la wadau wa mifugo na uvuvi hufanyika kila siku kwenye banda la wizara ya mifugi na uvuvi kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.