Home Mchanganyiko IGP SIRRO: TUKO TAYARI KUKABILIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU.

IGP SIRRO: TUKO TAYARI KUKABILIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU.

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Mratibu
Mwandamizi wa Programu za Mafunzo ya Kuzuia uhalifu Unaovuka Mipaka
Bwana Willem Els (kulia), kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama nchini Afrika
ya Kusini wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya
kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Robert Boaz (wa pili kulia) wakati akito neno
mbele ya Wajumbe kutoka Kituo cha Ufanisi cha Kuzuia na Kupambana na
Ugaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kilichopo Nairobi nchini Kenya,
wakati Ujumbe huo ulipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya
kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai CP Robert Boaz, wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe
kutoka Kituo cha Ufanisi cha Kuzuia na Kupambana na Ugaidi katika Ukanda wa
Afrika Mashariki kilichopo Nairobi nchini Kenya, wakati walipomtembelea
ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo kwa lengo la
kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.