Home Mchanganyiko Wafanyakazi wa TBL waendelea kupata mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia

Wafanyakazi wa TBL waendelea kupata mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia

0

Afisa kutoka Jeshi la Polisi -Dawati la Kijinsia ASP Fatuma Mtalimbo, akitoa mada kwa wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa mafunzo kuhusiana na  kupinga vitendo vya  ukatili wa kijinsia kwenye jamii  yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki.

Afande Fatuma Mtalimbo akiwa katika picha na wafanyakazi wa TBL baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

***************

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL) mwishoni mwa wiki walipatiwa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia  kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya kijinsia wa Jeshi la Polisi-Dawati la Jinsia ASP, Fatuma Mtalimbo.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa kampuni kuvalia njuga suala la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na taasisi za Serikali na wanaharakati mbalimbali wa masuala ya jinsia.

Meneja Mawasiliano wa TBL, Abigail Mutaboyerwa, alisema kwa kipindi cha miaka mitatu sasa Kampuni ya TBL  imekuwa ikishirikiana na wadau wanaoendesha harakati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kupitia kampeni yake inayojulikana kama #NoExcuse# .

“Suala la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, TBL itaendelea  kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kuelimisha jamii kutumia vinywaji vyenye kilevi kistaarabu na kuacha dhana na visingizio kuwa matumizi yake ndio yanapelekea watumiaji kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia” alisema Mutaboyerwa.

Alisema kampuni ya TBL inaamini kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaweza kutokomezwa kwenye jamii iwapo kila mtu atavikemea na kuchukua hatua kwa kushirikiana na taasisi za Serikali na kusisitiza kuwa elimu waliyopata wafanyakazi itawanufaisha binafsi sambamba na kuifikisha kwenye jamii.