Home Mchanganyiko MBUNGE ARUMERU MASHARIKI KUSHIRIKI UJENZI WA JIKO NA BWALO SEKONDARI YA LEGURUKI

MBUNGE ARUMERU MASHARIKI KUSHIRIKI UJENZI WA JIKO NA BWALO SEKONDARI YA LEGURUKI

0

************

Na Ahmed Mahmoud Arumeru

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru mashariki, Dakta John Pallangyo, ameahidi  kushiriki ujenzi wa Jiko na bwalo la  Chakula la shule ya sekondari Leguruki,ambayo ni shule pekee inayomilikiwa na Jumuia ya wazazi ya Chama cha Mapiduzi ccm mkoa wa Arusha .

Mbunge huyo ambae alikuwa ni mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Jumuia ya wazazi mkoa Arusha, ambayo yalifanyika  kwenye Viwanja vya shule ya Leguruki, wilayani Arumeru ,ambpo alisema kuwa anatambua changamoto inayoikabili shule hiyo ambayo ni Jiko na bwalo la chakula.

Alisema atashirikiana na uongozi wa shule pamoja na wazazi wa watoto wa shule hiyo kuhakikisha majengo hayo yanakamilika ndani ya muda mfupi  na kuwezesha wanafunzi kupata huduma stahiki  na hivyo kuwawezesha kuongeza ufaulu kwenye masomo yao.

Mbunge huyo ambae ni mwenyekiti mstaafu wa Jumuia ya wazazi mkoa wa Arusha, aliwataka wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuongeza bidii ili yapatikane matokeo mazuri  na kuifanya shule hiyo iwe miongoni mwa shule bora nchini zenye matokeo mazuri ya kidato cha nne na sita.

Pallangyo, alisema kuanzia mwaka huu hataki kusikia shule hiyo inakuwa na matokeo mabovu bali iwe ni miongoni mwa shule zinazoongoza kwa kuwa walimu  wapo wanafunzi wapo na vifaa vyote vipo hivyo haoni kwa nini isiwe na matokeo mazuri.

Aliwataka wanafunzi hao kutambua kuwa wameenda shuleni kusoma na sio kucheza disiko na wakifanya vizuri wataipatia soko shule hiyo.

Awali mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi mkoa wa Arusha Hezron Mbise, alisema kwenye maadhimisho haya  ambayo yalizinduliwa wilayani Monduli wiki iliyokwisha  wameweza kupokea mizinga ya 50 nyuki kutoka makao makuu ya Jumuia hiyo pamoja na wadau  ambayo itagawanywa kwa wilaya zote saba za mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi .

Kuhusu kero zilizoko jimboni humo mbunge huyo ameanza ya kutembelea kata zote na kushirikiana na wananchi katika utatuzi wa kero zilizopo.

Alisema anatambua Jimbo hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo atazitatua kwa kushirikiana na wananchi pamoja na serikali kuu na halmashauri ya wilaya hiyo

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Uchumi mipango na fedha wa Jumuia hiyo mkoa wa Arusha, Liliani Mtiro, alichangia shilingi 500000 na kuahidi kumalizia shilingi 150,0,000 kwa ajili ya ujenzi wa jiko na bwalo la shule hiyo .

Mtiro aliungwa mkono na mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi mkoa Hezron Mbise aliyechangia mifuko 100 ya Saruji huku Mbunge wa Jimbo hilo Dakta Pallangyo amechangia mifuko 150 ya Saruji.