Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (kulia) akizungumza wakati alipotembelea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Mkuu wa miradi wa Taasisi Islamic Help Tanzania akieleza kazi zinazofanywa na Taaisis yake kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipotemblea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akishuhudia shughuli zinazofanywa na Taasisi Islamic Help Tanzania kwa njia ya video wakati alipotemblea Taasisi hiyo inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Wadau kutoka Taasisi ya Islamic Help Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu( hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipotemblea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Taasisi ya Islamic Help Tanzania wakati alipotemblea Taasisi hiyo inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
*************
Na WAMJW- TANGA.
Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini imewafuta machozi wananchi wa mkoa wa Tanga kwa kuwasaidia kujenga miradi ya maji iliuohusisha visima 200 kwa Wilaya za Pangani, Mkinga, Handeni, Lushoto jambo lililosaidia kipunguza hadha kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo mkoani Tanga na Mkuu wa miradi wa Taasisi hiyo Bw. Amjad Khan wakati alipopokea ugeni kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu aliyeongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tanga.
Bw. Amjad Khan amesema kuwa Taasisi ya Islamic Help Tanzania imejipanga katika kuisaidia Serikali kupambana dhidi ya umasikini kwa kuwasaidia wananchi katika nyanja mbali mbali hususan katika Elimu, Uchumi, Afya, Malezi ya Watoto yatima, Mazingira.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo inatoa msaada wa chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kila mwezi kwa miezi miwili kwa wilaya ya Pangani, na kwa eneo la Rufiji huwa wanapokea pesa taslim kwa ajili ya kununu chakula.
Bw. Khan amesema mbali na misaada hiyo pia Taasisi yake inatoa huduma za afya hasa huduma za Afya ya macho kwa kuweka kambi za upasuaji wa mtoto wa jicho katika mkoa wa tanga na huduma hizo hutolewa bure kwa wananchi.
Aidha Bw. Amjad Khan alisema kuwa Taasisi hiyo imesajiliwa kama Taasisi ya kiislam inayosaidia binadamu wote na sio kuwa lengo la kuwasaidia waislam pekee hasa kwenye ibada kwa misikiti, huku ikitoa chakula kwa masikini mwezi wa ramadan.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ameishukuru taaissi hiyo kwa kujikita katika kusaidia wananchi hasa wale wa hali ya chini kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya, maji, Elimu na malezi kwa watoto yatima.
Waziri ummy ameongeza kuwa Serikali ipo pamoja na Taasisi hiyo na Taasisi nyingine zote zinazofanya mambo kama hayo ya kuisaidia jamii ya watanzania kujikwamua kiuchumi na kutoa huduma za kijamii.
“ Niwapongeze Taasisi ya Islamic Help Tanzania amejitoa kusaidia kaya maskini naamini zitajitokeza Taasisi nyingine ziige mfano wenu huu bora wa kuisadia jamii ya watanzania” alisisitiza Waziri Ummy.