Home Mchanganyiko TCRA Kanda ya Mashariki katika maonesho ya Nane Nane Morogoro

TCRA Kanda ya Mashariki katika maonesho ya Nane Nane Morogoro

0

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akiwa katimu picha  ya pamoja  na timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Christopher John akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Mwananchi akisaini kitabu wakati alipotembelea banda la TCRA kanda ya  Mashariki katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Wananchi wakipata huduma katika banda la NIDA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

Baadhi ya watoa huduma za Simu katika Banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

************

Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani Kanda ya Mashariki (TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Mashariki watumie maonesho ya Nane Nane  kupata elimu ya Mawasiliano pamoja  uhamasishaji wa usajili wa laini za simu  kwa alama za vidole.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero katika  Maonesho ya Nane Nane Kanda ya mkoani Morogoro, amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.

Mhandisi Odiero amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka  huu.

Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba na kufanya watu wengine kuona muda uliopangwa ulikuwa hautoshi.

“Muda uliowekwa ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu  hizo. 

Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalilbali za amawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.