Home Mchanganyiko MHANDISI METHEW MTIGUMWE AYATAJA MAONESHO YA NANENANE KUWA TASWIRA CHANYA KWA WAKULIMA

MHANDISI METHEW MTIGUMWE AYATAJA MAONESHO YA NANENANE KUWA TASWIRA CHANYA KWA WAKULIMA

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew J. Mtigumwe akisikiliza maelezo kuhusu Taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi kwenye Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

SHEREHE za wakulima maarufu
kama Nane Nane zimetajwa kuwa ni darasa huru kwa wakulima, wadau wa kilimo na
wananchi kwa ujumla kwani zinatoa nafasi kwao kujifunza mambo mbalimbali
yahusuyo kilimo chenye tija, Ufugaji wa kisasa na Uvuvi wenye tija pasina kuharibu
rasilimali za serikali.

Hayo yamebainishwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew J. Mtigumwe wakati akizungumza
na mtandao wa Wazo Huru Blog mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya
Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi
kwenye Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Alisema kuwa serikali
inatambua kadhia inayowakabili wakulima nchini ikiwemo pembejeo feki ambazo
wakulima wanauziwa, hivyo kupata hasara ikiwamo mazao kidogo na hafifu tofauti
na kusudio lao la kujipatia mazao mengi ya biashara na chakula jambo ambalo
inalifanyia kazi ili kukabiliana nalo kwa haraka.

Maonyesho haya Kitaifa
yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yatawasaidia wakulima
kupata elimu juu ya pembejeo halisi ikiwamo mbegu, dawa (viuatilifu), mbolea
kutoka kwa mashirika husika yanayozalisha pembejeo mbali mbali, ili kuwasaidia
kuepuka kununua pembejeo feki ambazo huwasababishia hasara na kuwakatisha
tamaa.

Sherehe hizi huambatana na
maonyesho ya bidhaa za kilimo yanayofanywa na wakulima na mashirika mbalimbali
yanayojihusisha na masuala ya kilimo, lengo likiwa ni kujitangaza shughuli zao,
kubadilishana uzoefu na wataalamu wa kilimo.

Pia wakulima wadogo ambao
ni wengi ukilinganisha na wakulima wakubwa watajifunza mbinu mpya za kitaalamu
za kilimo zinazoendana na wakati uliopo kwa maana ya mabadiliko ya kiteknolojia
na tabia nchi ili wakulima waweze kulima kilimo cha kisasa na kunufaika
kiuchumi.

Mhandisi Mtigumwe alisema
kuwa Kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea ambacho
hakizingatii kanuni za kitaalamu, jambo lililowasababisha kukata tamaa na kuona
kuwa kilimo hakilipi kutokana na mbinu duni walizozitumia.

Alisema kuwa Wizara ya
Kilimo inajipambanua zaidi kumkwamua mkulima ili Wakulima nchini waondokane na
kilimo cha kubahatisha cha kutegemea mvua na badala yake wajikite katika kilimo
cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika, kinachoweza kuyabadilisha maisha yao
kiuchumi kutokana na mazao mengi watakayopata.

“Natambua kuwa zaidi
ya asilimia 80 ya Watanzania wanategemea sekta ya kilimo kama ajira yao Sehemu
kubwa ya kilimo ni cha wakulima wadogo wadogo ambao mashamba yao yana ukubwa wa
hekta 0.9 na hekta 3.0 kwa kila moja, Karibu asilimia 70 ya ardhi ya kilimo na
mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono, asilimia 20 hutumia maksai na
asilimia 10 hutumia trekta Hivyo kama wizara tutajitahidi kadri iwezekanavyo
kuwakwamua wananchi ili kuondokana na uduni katika mavuno” Alisema
Mtigumwe

Mbali na hayo, kilimo cha
Tanzania ni cha kutegemea mvua, uzalishaji wa mazao ya chakula ndio unaongoza
katika uchumi wa kilimo. Hekta milioni 5.1 zinalimwa nchi nzima kila mwaka,
kati ya hizo asilimia 85 ni kwa ajili ya mazao ya chakula tu, na wanawake ndio
wafanyakazi wakubwa mashambani.

Mhandisi Mtigumwe anasema
katika maonesho hayo anatarajia wakulima watajifunza mbinu bora na za kisasa za
kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Aidha ametoa  wito kwa
wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa
ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa
kilimo.