Home Mchanganyiko MBUNGE AMINA MOLLEL ATEMBELEA FAMILIA ZILIZOATHIRIKA NA MAJI YENYE MADINI YA FLOURIDE

MBUNGE AMINA MOLLEL ATEMBELEA FAMILIA ZILIZOATHIRIKA NA MAJI YENYE MADINI YA FLOURIDE

0

Maji yenye madini ya Flouride yame waathiri kwa kiasi kikubwa wakazi wanaoishi katika vijiji vya Losinoni Kati, Lemanda pamoja na vijiji vilivyopo katika Kata ya Oldonyosambu kwa muda mrefu sasa.

Maji hayo yamesababisha baadhi ya watoto na hata wazee ambayo wamepata ulemavu uliosababisha miguu kupinda.

Mbunge wa viti Maalum Amina Mollel ametembelea baadhi ya familia zilizoathirika na kujionea hali hiyo huku familia nyingi zikiwa katika dimbwi kubwa la umasikini.

Wakizungumza kwa furaha baadhi ya wakazi hao wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mradi mkubwa wa maji unaojengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 520 kwa kuwa utayanusuru maisha yao.

Tuwe na moyo wa upendo na kuwasaidia watu wenye uhitaji.