Home Mchanganyiko WAZIRI MWAKYEMBE AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUWEKA DARAJA NA SERIKALI

WAZIRI MWAKYEMBE AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUWEKA DARAJA NA SERIKALI

0

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe wakati akifungua  semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
……………………………………………
Serikali imewataka wamiliki wa vyombo vya habari kujenga daraja baina yao na serikali na kuacha kushirikiana na balozi za nje au taasisi za nje katika kujadili maslahi ya nchi
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es salaam, kwenye semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Mwakyembe amesema vyombo vya habari visiwe na hofu ya kushirikiana na serikali kwani wanapaswa kuweka daraja kati yao na kuachana na kuwa karibu na balozi au taasisi za nje.
Alisema wanatakiwa kutambua kuwa jambo lolote likifanyika nchini mtu wa kwanza awe serikali na siyo balozi za nje au taasisi za kimataifa.
“Tuwe na uzalendo kwenye, nchi yetu kwani jata nchi za nje hazitanngazi mambo mabaya ya kwao lakini wenyewe wanashinikiza kutangaza yetu,” alisema Mwakyembe.
Alisema hata gazeti likifungiwa au kupewa adhabu, wamiliki wanapaswa kuonana na waziri husika kwanza kuliko kukimbia kwa mabalozi au taasisi za nje.
Hata hivyo alisema hivi sasa hawezi kuzungumza na balozi yeyote wa nje ya nchi bila kuita waandishi wa habari wa hapa nchini.
“Sidhani kama kutakuwa  na jambo la siri ambalo watakuwa wanataka lisisikike na kuhitaji kuonana na mimi bila waandishi wa habari hivyo kuanzia sasa nitakukuwa nafanya hivyo,” alisema Mwakyembe.
Mmoja kati ya waandaaji wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Mac D, Deogratius Rweyunga alisema wanaendelea kufanya semina kama hizo ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari.
“Tulikuwa tunawajengea uwezo zaidi waandishi wa habari za michezo pekee lakini sasa tunafanya pia mafunzo kama haya na waandishi wa habari zote kwa mikoa mbalimbali,” alisema Rweyunga.
Akielezea mada katika mafunzo hayo mwezeshaji Allan Lawa alisema waandishi wanapaswa kuandika suluhu ya matatizo ya jamii na kubadilika na kuachana na kuandika matukio pekee.
“Tunapaswa kuzama kiundani kwa kuandika suluhu ya matatizo ili ajali, maradhi na mambo mengine na siyo kuandika tuu ajali inatokea sehemu kila mara au ugonjwa wa dengua unaua watu mikoa ya Dar es salaam na Tanga,” alisema Lawa.
Mmoja kati ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo, Joseph Lyimo kutoka kampuni ya Mwananchi, mkoani Manyara alisema amejengewa uwezo zaidi wa kuandika habari za changamoto na haki za binadamu.
“Nimejifunza mambo mengi mno hasa nafasi na wajibu wa uandishi wa habari za haki za binadamu na suluhisho la matatizi ya jamii kupitia uandishi wa habari na siyo kuandika matukio pekee,” alisema Lyimo.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe akisoma baadhi ya vifungu vya sheria ya Habari vilivyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakati akifungua  semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC akizungumza kuhusu semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Mkurugenzi wa kampuni ya MAC D ambayo ndiyo imeandaa semina hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bw. Deo Lweyunga akimshukuru Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wakati akuzungumza katika semina hiyo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.

Mwezeshaji wa semina hiyo Allan Lawa akiwasilisha mada katika semina hiyo.

Felista Mauya Mkurugenzi Ujengaji Uwezo wa Uwajibikaji akiwasilisha mada ya haki za binadamu katika semina hiyo.

Picha zikionesha washiriki mbalimbali kutoka vyombo vya habari waliohudhuria katika semina hiyo.