MWAMVUA MWINYI ,PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemkabidhi mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stephen Kebwe ambapo katika mkoa wa Pwani miradi minne iliingia dosari kwa kukataliwa kati ya miradi 95 yenye thamani ya sh.bilioni 40.436.
Kati ya miradi iliyokataliwa ni pamoja hospital ya wilaya ya Mafia ambayo ilitolewa kiasi cha
sh.mil403.600 na ujenzi wa barabara ya KN52 Kilimahewa huko Mafia yenye thamani ya mil.22.336 ambayo kalavati na barabara haina ubora na uendelevu wa mradi wa maji huko Bweni .
Mradi mwingine ni wa maji Bokomnemela,Kibaha Vijijini, baada ya kubaini taratibu za ujenzi kukiukwa katika zege la juu lililotengewa kiasi cha sh.milioni 1.5.
Akitoa taarifa hiyo ,wakati akikabidhi mwenge huo Mkoani Morogoro agost 2 mwaka huu, eneo la mpakani mwa mikoa hiyo Bwawani , Ndikilo alisema wilaya ya Mafia,Kibaha na mkoa kijumla umepokea maelekezo na wanayafanyia kazi.
Alifafanua tayari wamechukua hatua ya kuunda timu ya kufuatilia jambo hilo na ripoti itakabidhiwa kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).
“Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Pwani Julai 24 na kukimbizwa kwenye wilaya saba ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 imepitiwa yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 40.436.6:’, Kati ya miradi hiyo miradi 61 imekaguliwa,17 ilipaswa kuwekwa jiwe la msingi,9 kuzinduliwa na 8 kufunguliwa “alieleza Ndikilo.
Ndikilo alisema ,miradi hiyo ni mizuri lakini imejitokeza dosari ndogo ambayo wanaichukulia ni funzo na taratibu zinafanyika ili kutimiza maagizo waliyotakiwa kuyatekeleza .
“Nakupongeza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na timu yako, kwa kuwa makini kufuatilia thamani ya miradi na taarifa zake”” alisema Ndikilo.
Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea alitaka maelekezo aliyotoa yafanyiwe kazi.
Pia ,Mkongea aliupongeza mkoa huo kwa ushirikiano biana ya chama na serikali pamoja na viongozi wote kuwa na ushirikiano na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi na baadhi ya halmashauri kuinua mapato yake.
Licha ya mwenge wa uhuru kukataa baadhi ya miradi pia kiongozi huyo wa mbio za mwenge alinusa ubadhilifu wa fedha, katika mradi wa maji Ikwiriri huko Rufiji ambao umejengwa na mamlaka ya maji safi Dar es salaam DAWASA kwa zaidi ya sh.bilioni 2.055.6.