Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea vyerehani kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (wapili kushoto), vilivyotolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza kuzitumia katika kujiinua kiuchumi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi mmoja wa wananchi cherehani zilizotolea na Taasisi ya Islamic Foundation,kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo , Arif Nahdi,vyerehani hivyo vimetolewa kwa ajili wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi
Wananchi Visiwani Zanzibar waliogawiwa vyerehani na Taasisi ya Islamic Foundation wakiwa wamesimama mbele yake baada ya kuruhusiwa kuchukua.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza baada ya kupokea vyerehani tisini na nne kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (aliyekaa kulia), vilivyotolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza kuzitumia katika kujiinua kiuchumi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
……………………………
Serikali kuzilinda Taasisi za Kidini
Mwandishi Wetu
Serikali imesema itaendelea kuziunga mkono taasisi za kidini nchini ili ziweze kuleta maendeleo na kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni mdau muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kupokea msaada wa vyerehani Tisini na Nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne vilivyotolewa kwa taasisi ya TAYI inayojishughulisha na kuwaokoa vijana kutoka katika tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
“Serikali tumekua tukipokea misaada mbalimbali kutoka katika taasisi za kidini nchini,wamekua wakisaidia visima vya maji,mashule na kubwa zaidi wanafundisha maadili ili taifa letu liwe na watu makini wanaoweza kuliletea maendeleo siku za usoni,kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani tunaahidi kuzilinda taasisi hizi ili ziweze kufanya shughuli zake bila kubughudhiwa” alisema Masauni
Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa msaada huo wa vyerehani, Aref Nahdi amewaomba wananchi waliopokea mssada huo kwenda kuzitumia katika shughuli za ujasirimali akiamini watapata kipato zaidi endapo watazitumia vizuri.
“Nawaomba mkazitumie vizuri ili ziweze kuwaongezea kitu kwenye vipato vyenu,natoa wito msiende kuviuza kwani lengo lake ni kuwawezesha muwe na shughuli itakayowaingizia kipato na sisi kama taasisi tunaahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa wale wanafunzi ishirini wa kwanza watakaotaka kujifunza ushonaji ili waweze kuzitumia vizuri” alisema Nahdi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopokea misaada hiyo ya vyerehani wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa vyerehani hivyo huku waiwaomba wasichoke kuwasaidia mara kwa mara ili vijana wengi wawe na shughuli za kuzalisha kipato.