Meli ya mizigo ya MV Umoja iliyobeba mabehewa ya
treni yenye shehena ya mzigo wa Shirika la Programu ya Chakula Duniani (World Food Program-WFP) kutoka Mwanza kwenda Uganda iliwasili bandari ya Portbell, Uganda tarehe 31 Julai 2019.
treni yenye shehena ya mzigo wa Shirika la Programu ya Chakula Duniani (World Food Program-WFP) kutoka Mwanza kwenda Uganda iliwasili bandari ya Portbell, Uganda tarehe 31 Julai 2019.
Katika Halfa ya mapokezi ya meli hiyo, Serikali ya Uganda iliwakilishwa na Waziri wa Nchi-Uchukuzi, Mhe. General Katumba Wamala na kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Dkt. Aziz Mlima alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.
Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam hadi Kampala.
Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa kutumia njia hii wameokoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 2.
Ujumbe uliosafiri na meli ya MV Umoja iliyobeba mabehewa hayo yenye mizigo ya WFP ulijumuisha Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa; Mkurugenzi wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Johnson Kisaka ambao waliambatana na Mkurugenzi wa WFP-Tanzania, Bw. Michael
Meli ya MV. Umoja iliyobeba shehena ya mzigo, mali ya WFP kutoka Dar Es Salaam ikiwasili katika Bandari ya Port Bell jijini Kampala tarehe 31 Julai 2019. |
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima akitoa neno wakati wa hafla ya mapokezi ya meli ya Mv. Umoja jijini Kampala, Uganda. |
Balozi Mlima akiongea na wanahabari kuhusu zoezi hilo. |