NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(kulia),akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Ndugu Sunna Said Mzee(wa kwanza kushoto),Komputa hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).
VIONGOZI na Wanachama wa UWT wa Mkoa wa Magharibi wakiwa katika hafla ya kukabidhi komputa nne ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.
……………………..
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk,amewasihi Viongozi na Wanachama wa CCM kufanya Kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuandaa Mazingira rafiki ya Ushindi wa Mwaka 2020.
Rai hiyo aliitoa wakati akikabidhi Komputa Nne zenye Thamani ya Shilingi Milioni Nane kwa Ofisi za UWT Zanzibar ambazo ni Afisi Kuu ya UWT Zanzibar, UWT Mkoa wa Magharib,UWT Wilaya ya Dimani na UWT Wilaya ya Mfenesini ambapo kila Ofisi imekabidhiwa komputa Moja,Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za CCM huko Kiembembe Samaki Unguja.
Mhe.Amina alisema ili Chama kishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao kila mwanachama anatakiwa kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya maslahi binafsi.
Katika maelezo yake Mhe.Amina, alisema Vifaa hivyo ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa Wananchi.
Pamoja na hayo aliwaahidi Akina Mama wa Mkoa wa Magharibi kuwa ataanzisha Vikundi vya Ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi Wanawake hao.
Aidha alisema kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo hasa Wabunge na Wawakilishi watakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za Wananchi bila ubaguzi wa kisiasa,kidini na kikabila.
Aliwasihi Viongozi na Wanachama wa UWT kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Viongozi hao ili wazidi kupata nguvu na Uthubutu wa kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.
“Tukiwa Viongozi wa Mkoa huu kwa pamoja tutaendelea kushirikiana kwa kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi kubwa na kutatua changamoto mbali mbali za Wananchi” ,alisisitiza Mhe.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo,alimpongeza Mbunge huyo na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo, ambao wamekuwa karibu na Wananchi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya CCM.
Ndugu Tunu,aliwataka Viongozi na Watendaji waliokabidhiwa Komputa hizo kuzitunza vizuri ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuhakikisha shughuli za kiutendaji za UWT zinatekelezwa kwa ufanisi zaidi.
Alisema Viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kufuata nyayo za Viongozi Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa katika kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.
Awali Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid,alisema Umoja na Mshikamano ndio siri ya mafanikio ya kuimarika kwa Umoja huo.