Home Mchanganyiko WANANCHI WA KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUHUDHURIA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI...

WANANCHI WA KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUHUDHURIA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU

0

 

Timu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) katika picha ya pamoja kwenye banda lao lilipo katika uwanja wa Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo wanatoa elimu kuhusiana na masuala mbali mbaliikiwemo namna ya teknolojia ya Nyuklia inavyotumika katika sekta ya Kilimo,Maji na Mifugo na Mazingira na namna ya inavyosimamia na kuthibiti matumizi salama ya mionzi.

*************

Na mwandishi wetu
Wananchi wanaoishi mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa ya jirani ,wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Nyakibindi ili kujipatia elimu ya ya  namna ambavyo  teknolojia ya nyuklia inavyotumika katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo kilimo, mifugo, maji pamoja na afya.
Akizungumza katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ,Afisa mwandamizi wa Utafiti wa TAEC,  Bwana Yesaya Sungita amesema kuwa wananchi watapata elimu ambayo itawawezesha kupata uelewa juu ya masuala ya matumizi salama ya teknolojia ya Nyuklia na udhibiti wake hapa nchi ili kutokuleta madhara kwa wananchi pamoja na mazingira.
Sungita amesema kuwa TAEC imekuwa ikihakikisha teknolojia ya Nyuklia inatumika ipasavyo katika sekta muhimu kama vile Maji, Mifugo na Kilimo.
Hata hivyo SUNGITA amesema mbali na wananchi kujua kuhusiana na teknolojia ya Nyuklia pia wataweza kufahamua namna TAEC inavyofanya kazi ya Kusimamia na kuthibiti matumizi ya salama ya mionzi nchini.