Mtaalam Mussa Otieno, Akitoa Elimu juu ya Mfumo wa iMES, kwa wataalam wa Jiji la Mwanza.
Wataalam wa Jiji la Mwanza wakiwa wanafatili kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Matoa mada juu ya Matumizi ya Mfumo wa iMES katika Ukumbi wa Jiji la Mwanza.
Mtaalam Ismail Chami akionekana kwa mbali amesimama akitoa maelezo juu ya ubora wa mfumo wa iMES utakavyokuwa suluhisho la taarifa huku wajumbe wakiwa wanafatilia kwa makini.
***********
Na. Atley Kuni- Mwanza
Mfumo jumuishi wa ufatiliaji na tathmini (intergration Monitoring and Evaluation System-iMES), umepokelewa vizuri na wataalam wa Jiji la Mwanza na kuuona kuwa mfumbuzi wa tatizo la taarifa na takwimu.
Wakizungumza katika kikao cha pamoja cha kuupitia mfumo huo kwa hatua za awali kwa maeneo ya majaribio kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa jiji la Mwanza, Mtakwimu Costantine Ruhinda na Afisa mazingira Fanueli Kasenene wote wa Jiji la Mwanza walisema, wanaiona iMES kama suluhu ya kudumu kutokana na historia isiyoridhisha ya masuala ya takwimu na taarifa katika kipindi cha nyuma kabla ya mfumo huu wa sasa.
Ruhinda alisema, wamekuwa na tatizo la kitakwimu kwa kupewa takwimu zinazo tofautiana ndani ya idara au sekta moja,
“Unaweza kupeleka dodoso asubuhi, ukirudi jioni kulifatilia ukapewa taarifa husika, halafu nadni ya muda mfupi siku inayofuata ukapeleke dodoso lingune, chakushangaza utakuta chanzo hicho hicho kimoja kimekupatia takwimu mbili tofauti ndani ya muda mfupi tu” alisema Ruhinda.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Jiji hilo, Fanueli Kasenene anaiona iMES kama suluhu ya tatizo lakunyang’anyana rasilimali hususan ni wakati wa upangaji wa vipaumbele vya bajeti.
“Sisi kama idara ya Usafi na Mazingra kipaumbele kikubwa kilikuwa kinaelekezwa kwenye Idara ya Afya wakati wa bajeti na hii ilitokana na idara hii ya Usafi wa Mazingira kuwa mpya na viashiria vya ukiutendaji vilikuwa vipo chini ya Idara ya Afya, hivyo basi kutotoa fursa yakutengeneza Mipango ikizingatiwa kuwa ni idara inayojitegemea” Alisema Kasenene.
Kasenene anasema, mifano halisi ilikuwa katika viashiria vya uzalishaji wa taka ngumu, viashiria vya uondoshaji na usafirishaji wa taka ngumu lakini pia viashiria vya maeneo ya wazi, maeneo yanayohifadhiwa (Environmental Protected Areas), kutooneka ndani ya Mifumo iliyopita.
iMES ni Mfumo ulibuniwa na kusanifiwa na Serikali kwakushirikiana na Wadau wa Maendeleo USAID chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS.3, kwakutumia wataalam wa ndani ya nchi.