Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Vicky Bishubo akikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo kompyuta, madaftari, na madirisha ya aluminum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kwenye shughuli iliyofanyika zahanati ya Nandangala wilayani Rukwa
Meneja wa Tawi la Ruangwa Abrahamu Eliakimu akimueleza Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kuhusu vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa na Benki ya NMB, NMB imetoa msaada wa thamani ya TZS 25 milioni
………………………
Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, kompyuta, na Madaftari vyenye thamani ya Tsh. Milioni 25 kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu na afya katika halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae pia ni Mbunge wa jimbo hilo katika Zahanati ya Nandagala iliyopo katika Kijiji cha Nandagala Wilayani humo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo alisema Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Madilisha ya Aluminium kwa ajili ya Zahanati ya Nandagala yenye thamani ya Tsh. milioni 15, mabati 56 zikiwa na Mbao zake za kupaulia vyenye thamani ya Tsh. Milioni 3.3, Kompyuta 10 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kasimu Majaliwa pamoja na Madaftali yenye thamani ya Tsh. Milioni 5 kwa ajili ya Shule mbali mbali katika Wilaya hiyo ya Ruangwa.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo kwa niaba Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Benki hiyo Albert Jonkergouw alisema kuwa kwa NMB changamoto za sekta ya Afya na Elimu hapa Tanzania ni jambo la kipaumbele kutokana na umuhimu wa sekta hizo kuwa ndio nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa.
“Sisi kama NMB tumekuwa msitari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii, ambapo kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tumeweza kuchangia 1% ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka” alisema Bishubo
Hata hivyo Bishubo aliongeza kuwa kwa mwaka 2019 Benki yao imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na Afya ambapo mpaka sasa tayari imeshatoa msaada wa zaidi ya Tsh. Milioni 600.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ikiwa ni moja ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano
Majaliwa alisema kama Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hivyo katika shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na majanga yanapotokea.