Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima kulia akipokea kadi ya Chama cha wananchi (CUF) kutoka kwa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) Akida Boramimi baada ya kujiunga na chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji
Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima kulia akipokea kadi ya Chama cha wananchi (CUF) kutoka kwa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) Akida Boramimi baada ya kujiunga na chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima kulia akimkabidhi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) Akida Boramimi baada ya kujiunga na chama hicho juzi kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo la sokoni wilayani Pangani Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima akizungumza wakati akimpokea aliyekuwa Diwani wa CUF Kata ya Pangani Mashariki Akida Boramimi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima akivishwa skafu mara baada ya kuwasili wilaya ya Pangani Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki Akida Boramimi(CUF) akizungumza ambapo alisema kasi na utendaji mzuri wa Rais Dkt John Magufuli umemvutia na kuamua kujiunga na CCM MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kushoto akimkabidhi vifaa vya kujikingia na jua ikiwemo kofia na vitu vingine kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani humo kiongozi wao kulia MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kushoto akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah mara baada ya kukabidhi baiskeli kwa watoto wenye ulemavu Sehemu ya wananchi wakimsikiliza MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki kupitia tiketi ya chama cha Wananchi (CUF) Akida Boramini ametangaza uamuzi wa kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).Akida alitangaza uamuzi huo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji uliofanyika eneo la Sokoni.Baada ya kutangaza uamuzi huo ambao uliibua shangwe na nderemo kwa wana CCM ambao walihudhuria mkutano huo na baadae kulazimika kutembea kwa maandamano mpaka zilizopo ofisi za CCM wilaya hiyo na kwenda kumkabidhi kadi.Diwani huyo ambaye ni mahiri kwenye kujenga hoja hususani anapokuwa kwenye vikao mbalimbali vya kimaendeleo kwenye baraza na hata vile vya kawaida alipofika kwenye ofisi hiyo alikabidhiwa kadi na Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira SilimaAlisema kwamba kubwa ambalo limepelekea kuamua kujiunga na chama hicho ni kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Dkt John Magufuli ya kuhakikisha wanatanzania wanapata maendeleo na ndio sababu iliyompelekea kuamua kuchukua maamuzi hayo“Kwa kweli Rais Dkt John Magufuli amefanya mambo mengi makubwa sana na ndio maana nimeona nimuunge mkono kwani kwenye masuala ya barabara na maji yanayopatikana hakuna haja ya kuendelea kuwa mpinzani…Lakini mimi niseme kwamba nimekuwa kada ya CUF tokea mwaka 1999 na ndio nimekabidhiwa kadi”Alisema“Lakini katika kuhamia CCM sijaja pekee yangu nimeambatana na wanachama wengine wa ACT akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi (ACT) Pangani Ally Mbwaro ,Wanachama kutoka Chadema na vijana wa bodadoda Pangani lengo kubwa ni kuhakikisha tunashirikiana kwenye hali ya kuijenga Pangani mpya”AlisemaAkida Borami ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Pangani alikuwa diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) tokea mwaka 2015akimshinda aliyekuwa mpinzani wake Leopard Abeid kwa kuwa zaidi ya kura 500.“Nimekaa nimejitafakari kwa namna mambo ya nchi yanavyokwenda nikaona sina budi kutangaza rasmi kurudi CCM na ni sikuja pekee yangu nimekuja na wenzangu wapatao 50 hivyo ninaomba mtupokee na kututhamini “Alisema.Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Pangani Aweso alisema kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imefanya mambo mengi makubwa ambayo yamekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa watanzania.Alisema kwamba tokea alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ameweza kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika wilayani humo ikiwemo kupandisha kiwango cha ufaulu kutoka kuwa wilaya ya mwisho kupanda kwenye nafasi za juu.Alisema pia licha ya hivyo lakini pia amesimama imara kwa kuhakikisha wanaanzisha madarasa ya kidato cha Tano na Sita hali ambayo imepelekea wanafunzi wanaofaulu kupata fursa ya kupata elimu.“Lakini pia niwaambie tumeweza kushghulikia kwa asilimia kubwa suala la maji ambapo mkataba wa milioni 575 umesainiwa kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji na utekelezaji wake umefikia asilimia 90”Alisema Mbunge Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji.