Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia)
akizungumza na askari na watumishi raia waliochini ya Wizara
yake, mjini Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro,
leo, akiwataka kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa. Pia
aliwataka viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuacha
tabia ya kuwanyanyasa watumishi, na pia wahakikishe
wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na
kulipwa fedha za likizo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),
akimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hassan Okello,
alipokua anatoa taarifa ya kikao cha askari na watumishi raia,
mjini Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, leo.
Lugola amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii bila
kukata tamaa. Pia aliwataka viongozi wa vyombo vya Ulinzi na
Usalama kuacha tabia ya kuwanyanyasa askari na watumishi
raia, na pia wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha
mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza
na askari na watumishi raia waliochini ya Wizara yake, mjini
Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, leo, akiwataka
kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa. Pia aliwataka viongozi
wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuacha tabia ya
kuwanyanyasa watumishi, na pia wahakikishe wanawapandisha
vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za
likizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),
akimsalimia Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Innocent
Magesa, wakati alipokuwa anawasili mjini Ifakara, leo kwa ajili
ya kufanya ziara ya kikazi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo,
James Ihunyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
**************
Na Felix Mwagara, MOHA-Ifakara.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka
viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya
Wizara yake nchini, kuacha tabia ya kuwanyanyasa askari
waliochini yao na wahakikishe wanawapandisha vyeo,
wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo.
Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili
kupandishwa vyeo na kurekibishiwa mishahara, kwa kuwa
Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli askari hao wana haki kwa
mujibu wa sheria.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi
wa Wizara yake, mjini Ifakara, Wilaya Kilombero, Mkoani
Morogoro, leo, Lugola alisema katika uongozi wake hataki
kusikia askari wananyanyaswa na kiongozi yeyote wa Taasisi
zake.
Lugola alisema, unyanyasaji, kutokupandisha vyeo, pamoja na
kulipwa fedha zao za likizo, changamoto hizo zinapunguza
nguvu ya utendaji kazi wa askari hao wanaofanya kazi ngumu.
Waziri Lugola aliongeza kuwa, alitoa agizo la askari
wanaostahili kupandishwa cheo, kurekebishiwa mishahara yao,
wanaodai kulipwa fedha za uhamisho pamoja na changamoto
mbalimbali zingine alizozielekeza.
“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara
yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini, lakini naamini kila kitu kinaenda vizuri na ahadi niliyoitoa
itakamilisha kwa wale askari ambao wanasifa watapewa vyeo
hivi karibuni,” Alisema Lugola.
Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi
ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli anatoa
mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna
upungufu mkubwa wa nyumba hizo.
“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la
ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali
inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,”
alisema Lugola.
Pia Lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari
wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na
atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi.
Lugola alisema jambo ambalo linamuumiza kichwa ni kuhusu
madai ya askari na watumishi wa wizara yake ambayo anasema
kama wafanyakazi hawatalipwa haki zao na utendaji wa kazi
utapungua.
Waziri Lugola yupo Mkoani Morogoro kikazi na tayari
amemaliza ziara yake Wilaya ya Kilombero, na anatarajia
kufanya ziara hiyo katika Wilaya za Malinyi na Ulanga Mkoani
humo.