Home Uncategorized Serikali Kutumia Maji ya Ziwa Victoria Kumaliza Tatizo la Maji Kanda ya...

Serikali Kutumia Maji ya Ziwa Victoria Kumaliza Tatizo la Maji Kanda ya Ziwa

0

Kaimu Meneja RUWASA Wilaya ya Mbogwe, Mhandisi Daudi Amlima akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso inayohusu Mradi wa Maji wa kisima kirefu wa Iboya uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Augustino Masele.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akifungua maji mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji wa Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulugala katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi mkoani Geita.

…………………

Serikali imejipanga kuachana na uchimbaji wa visima na kutumia maji ya Ziwa Victoria kikamilifu kwa ajili ya kupeleka huduma ya maji kwa wananchi kama suluhisho la muda mrefu la kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji.

Naibu Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji imeweka mkakati maalum wa kutumia moja kwa moja maji ya Ziwa Victoria hususan kwa eneo la Kanda ya Ziwa baada ya visima, ambavyo vimekuwa na changamoto mbalimbali zinazosababisha miradi yake mingi kutokuwa endelevu kwa kuwa maji yake si ya uhakika.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Iboya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Naibu Waziri Aweso amesema hakuna sababu ya kuendelea kuchimba visima kwa ajili ya wananchi waishio karibu na Ziwa Victoria wakati wana chanzo cha uhakika chenye maji ya kutosha.

‘‘Tumeweka mkakati wa kutumia Maji ya Ziwa Victoria na vyanzo vingine kikamilifu kupeleka huduma ya majisafi na salama kwa wananchi, mpaka sasa kwa uchache tumefanikiwa kufikisha maji kwenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu na tunaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa utakaopeleka maji kwenye miji ya Nzega, Igunga na Tabora Mjini kwa kutumia maji ya Ziwa Victoria, Naibu Waziri Aweso amesema.

‘‘Hakuna sababu ya kutumia fedha nyingi kwa kuchimba visima wakati tuna vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali, ukiacha maeneo yaliyo na uhaba wa vyanzo vya juu ya ardhi amb. Tumejipanga vizuri kutumia maji ya Ziwa Victoria, mito na maziwa mengine kumaliza tatizo la maji kaaytika Wilaya ya Mbogwe na maeneo mengine’’, Naibu Waziri Aweso amefafanua.

Aidha, Naibu Waziri wa Maji, Aweso amezindua Miradi ya Maji ya Lulembela na Bulugala yenye gharama ya zaidi Shilingi milioni 517 katika Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe inayohudumia wananchi 7,615.