Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Awali cha Magereza Kiwira, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Adriano Mduda akitoa taarifa fupi ya Chuo Ofsini kwake mbele ya Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akikagua gwaride la wahitimu wa Mafunzo ya Sajini wa Magereza Kozi namba moja jana Julai 26, 2019.
Mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo hayo Koplo Inocent Mutoka akivishwa cheo cha Sajini wa Magereza kwa niaba na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akimkabidhi cheti cha sifa mhitimu wa Mafunzo hayo, Koplo Mariam Mwakababile aliyefanya vizuri kwenye medani ya ulengaji wa shabaha jana Julai 26, 2019.
Kikundi namba tatu cha gwaride kikipita mbele ya mgeni rasmi katika mwendo wa haraka jana Julai 26, 2019.
Wahitimu wa Mafunzo hayo ya Sajini wa Magereza wakionesha umahiri wao katika onesho maalum la medani ya kujihami na adui jana Julai 26, 2019.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Julius Chalia(wa nne toka kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mathias Mkama, jana Julai 26, 2019