Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri
wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker mara baada ya
kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme
Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro
na Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe
Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri
wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker, Waziri wa Nishati
Medard Kalemani pamoja na viongozi wengine akisikiliza
namna mradi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo
la mto Rufiji utakavyokuwa ukifanya kazi mara baada ya
kukamilika.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed
Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi
mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika
eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia michoro ya
ujenzi huo mkubwa wa kufua umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Kuzalisha
umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakati
wakielekea kwenda kuweka jiwe hilo la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika mradi huo mkubwa
wa kufua umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la mradi huo wa umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi
mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi.
Eneo la mto Rufiji ambalo litatumika katika
ujenzi huo wa kufua umeme kama linavyoonekana. PICHA NA
IKULU