Baadhi ya Viongozi na watumishi Mkoani Tabora wakimsikiliza hivi karibuni Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Manispaa ya Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi.
Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiwahutubia wafanyakazi mkoani Tabora wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ili azungumze na wafanyakazi mkoani Tabora wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo akitoa taarifahivi karibuni kwa Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (wa pili kutoka kushoto) wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi.
……………………….
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imeipongeza Uingereza,kwa msaada wake katika sekta ya elimu ambapo imetoa zaidi ya Sh 600 bilioni kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE).
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi.
Alisema kuwa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE) ambao uliokuwa unafadhiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza,DFID umefanya kazi kubwa ya kuboresha elimu, miundombinu na kuboresha mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi.
Jafo alisema mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kujengwa miundombinu bora na wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na kuwapunguzia adha ya watoato kutembea umbali mfupi tofauti na zamani walipokuwa wakitembea umbali mrefu.
Aliitaka miradi inayoachwa na mpango huo wa kuboresha elimu iendelezwe na hatua zichukuliwe kwa wale watakaoihujumu.
Jafo alisema kuwa kumekuwepo na tabia katika baadhi ya maeneo ambapo wafadhili wanaposaidia miradi ya maendeleo , pindi wanapotoka na miradi inakufa jambo ambalo sio zuri.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa wameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanaweka katika bajeti zake vipengeleo vyote vilivyokuwa kuwa katika mpango ili kuhakikisha unakuwa endelevu.
Alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuihujumu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza,DFID,Beth Arthy alisema kuwa Uingereza imegharamia ujenzi wa madarasa zaidi ya 700 yaliyojengwa katika shule za msingi kwenye mikoa 9 ya Tanzania Bara.
Alisema madarasa hayo mapya yameongeza nafasi za masomo kwa zaidi zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo ujenzi wa madarasa hayo pia,ulihusisha ujenzi wa vyoo 1,300.
Alieleza kwamba ufadhili wa Serikali ya Uingereza ulipitia Mpango ya kuboresha elimu, ambao pamoja na ujenzi wa madarasa na vyoo,umetoa mafunzo kazini kwa zaidi ya walimu 50,000,walimu wakuu 5,000 na waratibu elimu kata 1,300.
Katika mkoa wa Tabora pekee,mradi huo umejenga madarasa 95,vyoo 176 na ofisi za walimu 32 huku ukitoa mafunzo kwa wakuu wa shule 773 na waratibu elimu kata 206
Beth alisema mpango huo umeleta mafanikio ambapo viwango vya ufaulu katika shule za msingi kwenye Mkoa wa Tabora,vimepanda kutoka asilimia 37 mwaka 2013 kabla ya mradi hadi asilimia 73 mwaka 2018.