Home Michezo Sensei Rumadha Fundi Jundokan Karate Na kufuzu Mtihan wa Dan ya...

Sensei Rumadha Fundi Jundokan Karate Na kufuzu Mtihan wa Dan ya 5 Godan

0

Baada ya kurudi nyumbani jioni ya leo toka mjini Vienna, Austria katika semina mahususi iliyoandaliwa na kushirikisha nchi 19 and washiriki wapatao 200 kusimamiwa na masters wa Jundokan toka Okinawa, Japan. Hatimae, sensei Rumadha Dan 5 ( Godan) alikuwa ni mmoja wa washiriki walioidhinishwa kufanya mtihani wa ngazi ya juu ya Dan ya tano kwa chama hicho.

Jambo ambalo la kuzingatia na kutafakarini kwamba, sensei Rumadha alianza mafunzo yake ya Karate katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililokuwa ndani ya shule ya secondary ya wasichana ya Zanaki mwishini kabisa mwa mwaka 1978 kwa muda mfupi na hatimae kurudi tena 1979 baada ya Sensei Bomani kutembelea na kuwafanyia mitihani wanafunzi wa Dojo hilo.
Sababu kubwa ya kutofautisha vyama tofauti vya mtindo mama wa Okinawa Goju Ryu ni jinsi gani wanafunzi wanatofautiana katika mbinu za ufanyaji Kata na mbinu mbalimbali toka shule moja hadi nyingine. Utakuta kwa mfano wake sensei Rumadha, ni kwamba, yeye alikwenda shule au Dojo alipojifunza Sensei Bomani huko mjini Naha, Okinawa na chini ya mfumo wa Master Eiichi Miyazato Hivyo basi, kufuatana na ngazi alizopitia na mitihani ya Jundokan chini ya mwenyekiti wa chama hicho Kancho Yoshihiro Miyazato, ndio kusema kwamba mafunzo hayabadiliki na ndio hayo aliyofundishwa hadi ngazi hiyo ya Godan.
Hivyo basi, ni change moto kubwa na kupotoshwa kwa myuyeyote anaesoma mbinu na Kata kupitia njia za mtandao sababu moja kubwa nikwamba upo uwezekano wa kuwa unafuata vyama kipofu bila kujua kata ipi inachezwaje na speed yake au mbinu zake zipo vipi endapo kama huna mwongozo sahihi kama aliyosoma yeye(Jundokan Asato Honbu Dojo) huko Okinawa Dojo maarufu toka mwaka 1957 kuliko zote za Okinawa. Kwa usemi huu, ni kwamba Sensei Rumadha anafundisha jinsi alivyosomeshwa na masters wa Jundokan Goju Ryu tu.

Sensei Rumadha anapenda kusisitiza kwamba, kwa wale wanao jifunza nusunusu toka mchanganyiko wa Goju Ryu tofauti, wanapoteza sana umadhubuti wa Sanaa hii ya Okinawa Goju Ryu. Ni lazima wachague mwenendo mmoja tu na kuweka juhudi zote kuelekea mfumo huo. Zipo aina mbalimbali za Goju Ryu, mfano wake : Jundokan Goju Ryu, ilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master Chojun Miyagi na haijabadilika chochote hadi hii leo.Meibukan Goju Ryu, ilianzishwa na Meitoku Yagi na inambunu na kata zinachezwa tofauti na ile ya Jundokan. Shoreikan Goju Ryu, ipo tofauti pia. Kyokai Goju Ryu inavijitofauti vya mbinu, ingawa asilimia 95 ni sawa na Jundokan. Goju Kai, inatofauti za nayo kwa kadri kubwa. Kyenkukai Goju Ryu, haina tofauti na Jundokan, ilianzishwa na mwanafunzi wa Eiichi Miyazato, Sensei Masaji Taira. Seiwakai Goju Ryu, inatofauti kidogo na Jundokan pia. IOGKF ilianzishwa na Morio Higaonna, na zipo tofauti wa Kata na Bunkai kidogo.

Master Chojun Miyagi, kabla ya kifo chake, alikuwa anasaidiwa na mwanafunzi wake mkuu ambae ni master Eiichi Miyazato mwanzilishi wa Jundokan, kwa sasa mwanae Kancho Yoshihiro anaendeleza utamaduni huo ukizingatia huyo ndio aliyesimamia mitihani ya sensei Rumadha Fundi na kudhihilisha kwamba ndie mwenye uelevu fasaha wa Jundokan Kata na Bunkai kwa hadui sasa jinsi Jundokan utalatibu wake (Sylllabus) ya ilivyo. Na kwa wale wote wana Goju Ryu wa Tanzania, hawanabudi kufahamu muhimili gani au upi wanaoshika na kusambaza kifanisi Sanaa hii bila ya kuyumba toka chama Fulani hadi kingine , eti sababu jina lake ni Okinawa Goju Ryu. Hiyo sio tija n ani mihimu kujua unaposimamia ni wapi, chama kipi na lengo kujua nini? La, upo uwezekano wa kuwa kama bendera tu popote upepo uendapo huko ndipo unapokwenda pia. Nasema haya sababu, tu Tanzania, lazima tuwe na utambulisho (Affiliation) na kuheshimika kimataifa. Kujua chama chako kwa umadhubuti na makao yake huko Okinawa, Japan.

Sasa ni takriban Zaidi ya miaka 40 ya mafunzo ya Karate ya Sensei Rumadha Fundi na anapenda kuwa hamasisha wana Karate kuwa na mwelekeo mmoja tu na sio kuyumbishwa na mifumo tofauti. Yapo mazoezi shirikishi, bila kurekebishana sababu kubwa ni vyama tofautiana hata kama jina ni Goju Ryu, lazima wanafunzi waweze chambu tofauti zake, ni jambo muhimu sana kwa wana Goju wote dunuani.

Mwisho natoa shukrani zisizo na mwisho kwa Kanco Miyazato na baraza lake lote la mbinu za Jundokan Karate kwa kunifanyia mtihani wa Godan miongoni mwa madaraja tofauti ya washiriki zaidi ya 25 toka ngazi ya mkanda kahawia hadi Dan ya tano mkanda mweusi. Shukran kwa masters wote walionisaaaidia kufikia ngazi hii leo.
Jundokan Karate, chini ya sensei Rumadha Fundi, imetambulika sasa ni tawi hai la Tanzania kwa mujibu wa Kancho Miyazato.