Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi,akimuapisha Rasmi Mkuu mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo,aliyeteuliwa jana na Rais Dkt.Magufuli kuchukua nafasi ya Miraji Mtaturu ambaye kachanguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CCM)
Mkuu Mpya wa wilaya ya Ikungi Bw.Edward Mpogolo,akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida,Bi.Rehema Nchimbi wa pili kushoto ni Kaimu Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati,Dodoma Bi.Jasmin Bakari baada ya kuapishwa rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi,akimkabidhi barua Mkuu mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo,aliyeteuliwa jana na Rais Dkt.Magufuli kuchukua nafasi ya Miraji Mtaturu ambaye kachanguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (CCM)mara baada ya kumuapisha rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Bi.Rehema Nchimbi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumuapisha Mkuu Mpya wa wilaya ya Ikungi Bw.Edward Mpogolo,kulia ni Kaimu Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kati,Dodoma Bi.Jasmin Bakari baada ya kuapishwa rasmi.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Ikungi Bw.Edward Mpogolo,akizungumz na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Bi.Rehema Nchimbi .
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Bi.Rehema Nchimbi,akiteta jambo na Mkuu Mpya wa wilaya ya Ikungi Bw.Edward Mpogolo,mara baada ya kumuapisha rasmi.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………………..
Na.Alex Sonna,Singida
MKUU mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo ameapishwa leo rasmi kuanza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya hiyo, kuchukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Miraji Mtaturu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu jana, uteuzi wa Bwana Mpogolo ulianza rasmi jana july 24, 2019, kuwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi, Mpologo ameahidi kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya katika kuhakikisha inakuwa na maendeleo sambamba na kusimamia kikamilifu makusanyo ili kuinua uchumi wa eneo hilo.
“Ninamskuru Rais Dk,John Magufuli kwa kuniteua,ninaahidi kuwa sitamwangusha ,nitahakikisha ninashirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri yangu ya Ikungi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya makusanyo katia Wilaya yetu”amesema Mpogolo.
Ameahidi kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili kuhakikisha wanatumikia wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa wao ndio wawakilishi wa Rais katika eneo hilo.
Pia ameahidi kwenda kuisimamia Katiba ya Nchi pamoja na Ilani ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi katika kuwatumikia wananchi atakaowaongoza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Sindida Dk. Rehema Nchimbi amesema Mkuu wa Wilaya ndio msimamizi mkuu wa Kamati ya ulinzi na usalama na ndio msimamizi mkuu wa shughuli za maendeleo katika eneo husika na kumtaka kwenda kusimamia vyema miradi ya Serikali inayotekelezwa Wilayani humo.
“Mkuu wa Wilaya yeye ni msimamizi mkuu na muwakilishi wa Rais katika Wilaya na ndio mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama na ukasimamie miradi yote inayotekelezwa Wilayani humo” amesema Dtk Rehema.
Hata hivyo amemwambia kuwa Wilaya ya Ikungi inamiradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kwenye malengo ikiwemo miradi ya visima 28 vilivyokusudiwa kukamilishwa .
Aidha Dk.Nchimbi amesema upande wa Singida magharibi wanamiradi ya visima 13 na Singida mashariki visima 15 .
Amebanisha malengo mengine yaliyowekwa kwa Wilaya hiyo kuwa ni kilimo cha zao la michikichi ekari 200 pamoja na kilimo cha zao la korosho.