Home Mchanganyiko RAIS DKT MAGUFULI APOKEA DHAHABU NA FEDHA ZILIZOKAMATWA NCHINI KENYA

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA DHAHABU NA FEDHA ZILIZOKAMATWA NCHINI KENYA

0

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea
kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma
Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye
hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
Jumanne Julai 24, 2019

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaidia kuhesabu vipande
vya dhahabu huku akishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi aliyevipokea kutoka kwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja
na pesa zilizokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya
makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai
24, 2019

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kushuhudia Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
Kabudi akipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi
Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa xzilizokamatwa katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka
Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar
es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu wa Rais
Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana kwa simu ya mkononi na Rais wa
Jamhuri ya Kenya Mhe Jomo Kenyatta baada ya viongozi hao kushuhudia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi akipokewa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi
zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019.
Kushoto ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akifuatiwa na Mhe
Monica Juma. Kutoka kulia ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko
akifuatiwa na Profesa Kabudi na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali
Mhe Biswalo Mgangha

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma baada ya kukabidhi Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019

PICHA NA IKULU

……………….

Na: Waandishi wetu,MAELEZO

DAR ES SALAAM

RAIS Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.

Amesema kuwa  Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo  kati ya Tanzania na Kenya,  na ameeleza kuwa  kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu na pesa  hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.

“Tunaipongeza  Serikali ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na  tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais Magufuli

Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na ukimya  kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa  Kenya na Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  ambapo watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.

 “Vyombo vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia  alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.

Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na  Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.