Home Mchanganyiko MLOGANZILA WAPATIWA MAFUNZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.

MLOGANZILA WAPATIWA MAFUNZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.

0

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene
(kushoto) akiwapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto
watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, kulia ni Mkaguzi
Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a.

Watumishi wa Hospitali ya Mloganzila wakifuatilia mafunzo hayo.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a
akielezea majanga ya moto yanavyotokea na namna ya kukabili.

Kamanda Shang’a akifundisha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa
kutumia blanket maalum ya kuzimia moto (fire blanket).

Kamanda Shang’a akielekeza namna ya kuzima moto kwa kutumia
kizimia moto aina ya poda kavu (dry powder fire extinguisher).

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi
la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya
majanga ya moto.

**********

Dar es salaam 24-07-2019

Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzo
ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa lengo la kujikinga na
majanga ya moto na kuhakikisha Tanzania inakua salama dhidi ya majanga ya
moto.

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo ni yanadharia na vitendo yametolewa na Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji.

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Peter Mwambene amesema moja ya vitu vinavyomfanya mtu ashindwe
kupambana na moto ni uoga na kutokua na vifaa sahihi vya kupambana na moto
unapokua katika hatua za awali.

Hivyo mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa matumizi sahihi ya vifaa vya
kuzimia moto, kujua aina mbalimbali za moto na namna ya kukabili, kujua mbinu
za kuzima moto pamoja na namna ya kujiokoa pindi moto unapotokea.

“Moto unapotokea mtu hushindwa kuukabili kutokana na uoga, unatakiwa ufanye
yafuatayo pindi unapogundua moto, piga king’ora, kengele au mayowe,ita Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji kupitia namba 114, watu wasiojiweza wapewe kipaumbele
kutoka eneo hatarishi, jaribu kuzima moto bila kuhatarisha usalama wako na watu
wengine’’ amesema Mwambene.

Ametaja vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha majanga ya moto kuwa ni
matumizi ya vifaa vya umeme visivyokua na ubora, ajali, nguvu asilia (radi,
upepo,mkali, tetemeko la ardhi , milipuko ya Volkano).