****************

NAIBU WAZIRI  wanchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge ,kazi  ajira na Wenye ulemavu   Mhe.Stella  Ikupa, ameitaka Manispaa ya Ilala ,kuharakisha  kuunda kamati  ili kurahisi utendaji kazi kutoka katika ngazi za mitaa na Wilaya.

Mhe. Ikupa ametoa  kauli hiyo  alipokutana na walemavu  Wilayani Ilala  akiwa katika ziara yake  ya kukutana na walemavu ambapo alisema  zimeundwa  Ilala  bado ikonyuma katiaka  kuunda kamati hizo kwani  mpaka sasa imeunda kamati  27 kati ya kata 36 na mitaa 76 kati ya mitaa 156.

“Fanyeni juhudi kubwa katika kuunda hizi kamati  zinaumuhimu mkubwa zitasaidia kuanzia huko chini kupata takwimu na siyo tu kwamba ziundwe bali zifanye kazi “

Aidha ameikumbusha Manispaa hiyo kutoa mafuta chupa moja kila baada ya miezi mitatu kwa watu wenye  Ualbino, na kuagiza mikokopo  ya asilimia mbili kwa walemavu iendelee kutolewa kwa utaratibu   uliowekwa badala ya kupewa kikundi  fulani ili kiwagawie wengine.

‘’Tayari tumesha weka kanunu za utoaji mikopo hii ,suala la kusema kipewe kikundi fulani  haliwezekani mimi ni mkweli nakwa wale mlichukua mikopo ya Bajaji mlitaka mpunguziwe rejesho nimezunguza na mkurugenzi amesema inawezekana mtakutana naye ili mliweke sawa’’Alisema  Ikupa

Pia alitoa rai kwa mkoa wa Dar es salaam ,kuviunga mkono vikundi vya wenye ulemavu  wanao tengeza vifaa saidizi  badala ya kuendelea kununua  kutoka nje  na kusema kuwa hata Rais Magufuli anasisitiza watanzania tupende vya kwetu ili kuendeleza viwanda vya ndani.

Ikupa  alisisitiza matumizi ya Lugha ya alama  pale mikutano inapofanyika  na pia katika mikutano ya kampeni za Serikali za mitaa  ili kusaidia  kundi hilo kumfahamu mtu anaye mpigia kura ,  pia akaagiza  kurekebishwa miundo mbinu ya majengo  kwa kwaajili ya walemavu   hasa yale ya  zamani yafanyiwe ukarabati.

Alisema Serikali kupita Ofisi ya Waziri mkuu imeendelea kuhakikisha kwa huduma kwa watu wenye ulemavu zinaendelea kuboreshwa na Wizara mbali mbali zimeendelea kutekeleza  na yameundwa madawati katika kila wizara na ofisi yake imeanza taratibu za kupata takwimu za wenye ulemavu kupitia  mitaa ili serikali iweze kupanga bajeti  kusaidia wenye ulemavu.

‘’Serikali pia tumeajiri watu wenye ulemavu wasiyo ona  ,tumeajiri  walimu 60 ,kwa hiyo  tunapo sema sekta binafs iajiri watu wenye ulemavu sisi lazima tuwe mfano”

Pamoja na hayo  Naibu huyo,  amewapongeza  watu wenye ulemavu kwa kuendelea kuwa watulivu na kusema kuwa matatizo ya na malalamiko yao kuhusu  kuvamiwa na watu wengine katika sehemu zao za kazi ya kuendesha bajaji zitafanyiwa kazi na Manispaa kwa  na kusema kuwa itafanika operesheni kubwa ya kuwaondoa watu wanao fanya kazi hizo katika maeneo ya walemavu bila utaratibu.

Kwa upande wao watu wenyeulemavu walio pata fursa ya kuzungumza katika  mkutano huo  pamoja na kumpongeza Naibu waziri , wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuwajali walemavu  na kuwapatia mikopo ya asilimia mbili , kuwawekea waziri anaye shughulikia masuala yao  jambo ambalo limewafanya kujisikia nao kama binadamu wengine.

“Hapo kipindi chanyuma,  Mlemavu alizaraulika  , alikuwa omba omba ,mchafu asiyekuwa  na mwelekeo  hata  hapakuwa  na hata Benk moja ambayo inaweza  kumkopesha fedha  leo Serikali ya awamu yatano  imetthamini sana Mhe Naibu waziri tupelekee pongezi zetu kwa  Rais wetu  mwambie tuna mpenda “ Alisema  Henry Chacha.