Waziri wa nishati Dr. Medard Kalemani amewatembelea wabunifu wa umeme walioitwa ikulu kutoka mkoani Njombe na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania miezi mitatu iliyopita na kutoa agizo kwa shirika la umeme nchini Tanesco kuwapa TRANSFOMA lenye thamani ya mil saba ,TABANI ambao ni mtambo wa kisasa wa kufua umeme wenye thamani ya mil saba pamoja na kusambaza nguzo katika vijiji vya wabunifu hao ili waweze kuzalisha zaidi na kunufaisha na watu wengine .
Dr Kalemani amefikia hatua hiyo baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa maagizo ya rais katika miradi ya umeme wa maji iliyobuniwa kienyeji na bwana John Fute maarufu Pwagu katika kijiji cha Msete na Rainel Ngailo katika kijiji cha Lugenge halmashauri ya mji wa Njombe ambapo baada ya ukaguzi huo alibaini kuwa endapo miradi hiyo itaboreshwa na kuendeshwa kisasa inaweza kuzalisha kiwango kikubwa cha umeme tofauti na sasa.
Amesema kilowati 28 zinazozalishwa na mzee fute aliyebatizwa jina la Pwagu kwa madai ya kwamba hajawahi kufanikisha jambo pamoja na kilowats 15 zinazozalishwa na mzee Rainel Ngailo katika kijiji cha Lugenge endapo miundombinu ikiboreshwa wabunifu hao watakuwa na uwezo wa kuzalisha MEGAWAT moja ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya nyumba 800.
Kufuatia maagizo hayo kwa tanesco wabunifu hao ambao ni mzee john Fute(Pwagu) na Rainel Ngailo wanashindwa kuzuia hisia zao na kutoa shukrani kwa rais Magufuli kwa kuwatambua kwa kuwa wameanza kubuni miradi yao kwa kuokota nyaya na vyumba ili kuunda mitambo yao na kuiomba serikali kuendelea kuwatambua wabunifu wengine .
Katika hatua nyingine Waziri Kalemani ameiagiza TANESCO kumsomesha VETA mtoto Julias Kibumo(14) ambaye ni mjukuu wa mzee Fute pamoja na mtoto wa mzee Ngailo ambao wameonekana kuwa na vipaji vya ubunifu kama wazazi wao ambao kwa nyakati tofauti wanaeleza kazi zao vijana hao.
Awali timu iliyotumwa na rais kuwatembelea wabunifu na kuangalia miundombinu wanayotumia , kuwapa ushauri wa kitaalamu pamoja vifaa vya kisasa ilitoa maagizo kwa shirika la TANESCO kuwa kuwapa nguzo na nyaya za laini za umeme jambo ambalo limetekelezwa na shirika hilo.
Katika ziara hiyo waziri pia amekagua utekelezaji wa miradi ya REA wilayani Makete na Kuwasha umeme katika kijiji cha Ndulamo,Ukwama na Ihela na kumtaka mkandarasi kumaliza usambazaji wa umeme vijijini ifikapo desemba mwaka huu.