MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali ya Buchimwe Cup 2019 akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili za Buigiri Mission na Songambele kabla ya fainali ambapo Buigiri Mission waliibuka mabingwa wapya kwa kuwachapa magoli 4-1 Songambele kwa mkwaju wa Penalti.
Wachezaji wa timu ya Songambele wakisalimiana na wachezaji wa Buigiri Mission kabla ya Fainali ya Buchimwe Cup 2019 ambapo Buigiri waliibuka mabingwa kwa kuwachapa Penalti 4-1.
Wamuzi wakiwa na manahodha wa timu za Buigiri Mission na Songambele katika fainali ya Buchimwe Cup 2019 ambapo Buigiri Mission waliibuka mabingwa kwa kuwachapa 4-1 kwa njia ya Penalti.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,akifurahi jambo na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi ambaye aliandaa mashindano ya Buchimwe Cup 2019 alipowasili kushuhudia Fainali baina ya Buigiri Mission na Songambele.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,akisalimiana na baadhi ya viongozi waliohudhuria fainali ya Buchimwe Cup 2019 iliyoandaliwa na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,(katikati) akishuhudia Fainali ya Buchimwe Cup 2019 kati ya Buigiri Mission na Songambele ambapo Buigiri waliibuka mabingwa wapya kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele kwa mikwaju ya Penalti akiwa na Diwani wa kata ya Buigiri kulia Mhe.Yindi ambaye ndo muandaaji wa michuano hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi wa kwanza kulia ambapo timu ya Buigiri Mission waliibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo kwa kuichapa 4-1 Songambele kwa Mikwaju ya Penalti,shujaa akiwa golikipa wa Buigiri akipangua mashuti matatu ya Songambele.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,akitoa zawadi kwa baadhi ya wachezaji walioibuka wachezaji bora wa Mashindano hayo ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi ambapo timu ya Buigiri Mission iliibuka kuwa bingwa kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele kwa mikwaju ya Penalti.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga,akimkabidhi Kombe Nahodha wa Buigiri Mission baada ya kuibuka Mabingwa wapya wa Buchimwe Cup kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele katika Fainali hiyo.
Wachezaji wa Buigiri Mission Mabingwa wapya wa Buchimwe Cup 2019 wakishangilia na Kombe lao baada ya kuichapa magoli 4-1 Songambele kwa Mikwaju ya Penalti.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………………
Na.Alex Sonna,Chamwino
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga amesema kuna haja ya walimu wa timu za Taifa kuangalia vipaji ambavyo vinapatikana maeneo ya vijijini.
Hayo ameyatoa wakati akifunga mashindano ya Buchimwe Cup 2019 yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Buigiri ambapo mchezo wa fainali ulizikutanisha timu za Buigiri Mission na Songambele.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema vijijini kumekuwa na vipaji vya hali ya juu lakini anakosekana mtu wa kuwashika mkono hivyo akawaomba walimu wa timu za Taifa kufika katika maeneo hayo.
“Waje na hapa kwetu Chamwino kuna vipaji vya hali ya juu naamini hata wale Algeria waliochukua AFCON kupitia vipaji hivi ninavyoviona hapa wasingeweza kutufunga,”amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi ambaye ndiye muandaaji wa mashindano hayo amesema ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ya Michezo wilayani humo ili kukuza vipaji vya vijana kwani Michezo imekua ni ajira kubwa iliyobadilisha maisha ya vijana wengi.
” Mhe DC tunakushukuru sana kwa kufika pamoja na kufanikisha mashindano haya bado tunakabiliwa haswa na uhaba wa viwanja pamoja na vifaa vya Michezo, tuwaombe Serikali kuwekeza Kwa nguvu pia huku vijijini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi,” amesema Mhe Yindi.
Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa,Joel Mwaka (CCM),Buigiri Mission waliibuka na ushindi wa Penalti 4-1 dhidi ya Songambele mara baada ya dakika 90 timu hizo kutoka sare ya kutofungana.
Aidha Wachezaji wote wa timu nane zilizoshiriki mashindano hayo wameweza kupatiwa Bima za afya 159 kwa kila mchezaji aliyeshiriki.
Bima hizo za Shirika la CHF ambazo Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi ameweza kuwapatia ili ziweze kuwalinda katika afya zao hivyo michezo ni Afya.
Jina la mashindano hayo,Buchimwe ni muunganiko wa herufi za mwanzo za vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Buigiri ambavyo ni Chinangali 2,Buigiri na Mwegamile.