Picha ikionyesha Muendesha mashine ya kuchanganya sege kutoka kampuni ya ukandarasi ya Booygues , Dominic Heriman akimuonyesha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga jinsi wanavyochanganya sege kwa kutumia komputa wakati katibu alipofanya ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 hapo ni ndani ya store yard ya Lot T2 iliopo katika kijiji cha Nanja .
Picha ikionyesha meneja wa mradi kutoka kampuni ya Booygues Energies &services Potier Mathiew akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye pamoja na viongozi mbalimbali wa Tanesco wakiwemo wakandarasi wakati walipotembelea moja ya shimo lililopo tayari kwa ajili ya kusimamisha mnara.
Picha ikionyesha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi
Picha ikionyesha mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye akimfafanulia jambo Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi alipotembelea na ukagua ujenzi wa Lot T1 iliopo Nangwa .
…………………..
Na Woinde Shizza ,Arusha
Serikali imesema imeridhishwa na kasi ya wakandarasi wanaojenga Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa kilovolti 400 inayopita katika mikoa ya Singida Babati , Arusha hadi Namanga kwani unaenda mbio na mpaka sasa asilimia 51 ya ujenzi imeshakamilika .
Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 ambapo ziara hiyo ilihusisha kukagua njia ya umeme ya Namanga ,kituo cha kupoozea umeme cha Legur kilichopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Arumeru , pamoja na njia za kusafirishia umeme zilizopo katika halmashauri ya Babati vijijini katika kijiji cha Nagwa .
Alibainisha kuwa kazi zinazofanywa na wakandarasi waliopewa miradi hiyo amerizishwa nazo sana na kasi wanayoenda nayo kwani hadi sasa wameshafanya kazi kubwa na asilimia 51% ya ujenzi wa mradi huo imekamilika hivyo asilimia 49 %tu ndio zimebaki na anaamini wa kasi wakandasi hao wanayoenda nayo watakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa ambapo alisema kuwa mradi huo unatakiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa serikali mwezi Aprili 2020 .
“nimepita nimeangalia hatua iliofikia mradi huu wa njia ya usafirishaji wa umeme ambao miundombinu hii itaunganishwa katika vyanzo vya uzalishaji umeme ,kwa iyo miundombinu hii ni muhimu sana ,na nia ya ziara hii ni kuangalia tumefikia wapi hadi sasa hivi pia kingine ni kuangalia kama kunachangamoto zozote zinazoikabili mradi ili kama zipo serikali tuweze kuzitatua lakini tatu kuangalia kama wakandarasi wanafanya kazi zao vizuri kwaiyo hayo ndiilikuwa sehemu kubwa ya lengo la ziara hii sasa nimetembea nanapenda kusema nimerithishwa sana na utendaji wa wakandarasi hawa kwani mapaka sasa hivi wameshasimamisha minara zaidi ya mia moja kati ya minara 384 itakayo simamishwa sehemu zote lakini pia misingi imeshawekwa kwa ajili ya ujenzi wa minara yote pia nimerizishw a kuona wakandarasi wote wameshafika saiti kulingana na Ratiba inavyosema”Alisema Luoga
Alisema katika mradi huu kuna Lot T5 ambayo ya kwanza inaanzia Singira mpaka Babati na Lot T2 ya pili inaanzia Singida hadi Arusha na Lot T3 ya tatu inaanzia Arusha mpaka Namanga ,Lot T4 inausisha ujenzi wa vituo vya kupooza umeme ambapo kimoja kiko kisongo na kingine kitakuwepo pale Singida na Lot T5 itahusisha kusambaza umeme katika vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi ,alisema kuwa kulingana na kasi ambayo wakandaras hawa wanaendanayo kunauwezekano mkubwa wa mradi huu kukamilika kabla ya ratiba iliyopangwa au utakamilika kwa wakati na mradi huu unahusisha ujenzi wa kilometa 400 kutokea Singida mpaka Namanga ,ambapo alibainisha kuwa serikali itahakikisha vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi huu vinapatiwa umeme huku akisisitiza kuwa hakuna hata kijiji kimoja ambacho kitarukwa.
“ Sisi kama serikali tumewaagiza wakandarasi hawa wafanye kazi kila siku,wakandarasi wawatumie vijana wetu katika kazi zote kazi ambazo zinaitaji elimu na hata zile ambazo aziitaji elimu na katika swala hili napenda kuwapongeza wakandarasi maana wametii maelekezo ya serikali na wameajiri vijana zaidi ya 400 ambao wanatoka katika vijiji ambavyo miradi imepita kuanzia pale ulipoanzia Namanga hadi Singida ,pia tumewataka wakandarasi washirikiane najamii zinazozunguka miradi hii ili kusiwepo na changamoto na katika hili tumewaambia wakiwahusisha wananchi katika swala la ulinzi wa miundo mbinu hii na hata katika zile kazi ambazo zitaweza kuwapatia kipato hawa wananchi wetu ili wao wao wananchi waweze kuwa walinzi wa mradi huu ,pia tumewaagiza wasimamie mradi uweze kukamilika katika viwango vinavyotakiwa ‘’Alisema Luoga
Kwa upande wake mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye alisema kuwa aliwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hawa ikiwa ni pamoja na kuwasadia kazi mbalimbali za ujenzi ,lakini pia alisema serikali imewahaidi wakandarasi hawa kuwasaida vitu mbalimbali kwa wakati ikiwemo kutoa vifaa vya ujenzi bandarini kwa wakati pamoja na kuwasaida vitu mbalimbali ambavyo wakandarasi hao watakamwa ili tu wakamilishe mradi huo kwa wakati
Alisema kuwa kukamilika kwa miradi hii itasaidia kuchochea maendeleo ya vijijini na mijini pia itaongeza pato la nchi yetu kwani tutaweza kuingia katika sera ya uchumi wa viwanda na wawekezaji wataweza kuja kwa sababu watakuwa na uhakika wa uwepo wa umeme lakini pia alitumia mda huo kuwashukuru vingozi wanaotembelea mradi huo na kuangaia mwenendo wa kazi ,na maendeleo ya kaz i , waliahidi kufanya kazi kwa bidii kwa uhadilifu na kuhakikisha mradi unakamilika kwa muda ambao umepangwa na kwa fedha ambayo imepangwa kutumika ambapo alisema kuwa hadi kukamilika kwa mradi huu unatarajiwa kutumia dola za kimarekani milioni 258 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 600