Home Mchanganyiko Milioni 150 zagharamia Mkutamo Mkuu wa ALAT kwa Miaka mitano Mwanza

Milioni 150 zagharamia Mkutamo Mkuu wa ALAT kwa Miaka mitano Mwanza

0

Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi (Kushoto) akikabidhi mfano wa Hundi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mh Gulamhafeez Mukadam ikiwa ni ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wa pili kushoto ni Mkuu wa KItengo cha Huduma za Serikali – NMB – Vicky Bishubo na Katibu Mkuu wa ALAT – Elirehema Kaaya. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.

******************

 Benki ya NMB imesaidia Zaidi ya shilingi Milioni 150 kwaajili ya Mikutano Mikuu ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo huku
wakiahidi kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa nchini kutatua changamotoi
mbalimbali.

Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi aliyasema hayo juzi
jijini Mwanza wakati akikabidhi udhamini wa Benki hiyo kama mdhamini Mkuu wa
wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT unaoanza leo katika Hoteli ya Malaika
Beach jijini Mwanza.

Mponzi alisema kuwa Benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopo
kati ya NMB na ALAT kupitia Zaidi ya halmashauri 180 ambapo Benki inashiriana
kukusanya mapato ya Serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni mmbia
wa karibu na serikali, hivyo mahusiano ya NMB na ALAT yameanza muda
mrefu uliopita.

“Tunaishukuru sekretariet ya Alat pamoja na wajumbe wote kwa kuendelea
kutoa ushirikiano, kufanya biashara pamoja na sisi kama benki tumekuwa
tukiendelea kuboresha huduma zetu ili kuweza kuhudumia serikali kuu
pamoja na serikali za mitaa,” alisema Mponzi.

“Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku tukizifikia Zaidi ya halmashauri 180
tukiwahudumia katika Nyanja mbalimbali za kibenki kuanzia wafanyakazi,
wafanyabiashara na wajasiliamari na pia madiwani nah ii inaonyesha utayari
wetu wa kuhudumia Serikali za mitaa.” Alisema Mponzi.

Mwenyekiti wa ALAT taifa – Gulamhafeez Mukadam ameishukuru Benki ya NMB
kwa kuonyesha kujali Serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonyesha
dhamira na ushirikiano wa kweli kati ya taasisi mbili.

Mheshimiwa Mukadam aliongeza kuwa jamii za Serikali za mitaa na mamlaka zake
bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono na
taasisi kama NMB kwaajili ya kusaidiana kutatua changamoto hizo.

Aliiomba pia Benki ya NMB kuangalia namna ya kuangalia upya misaada yake
inayotolewa kwa jamii kupitia uwajibikaji kwa jamii (CSR) akiomba Benki kuanza
kusaidia jambo ambalo mwisho linakuwa kubwa kuliko misaada midogo midogo
ambayo inaweza ikawa na mchango mdogo kwenye jamii.

Mukadam alitoa mfano wa misaada ya vifaa vya ujenzi mashuleni na
mahospitalini na kusema kuliko kusaidia vifaa vya kuezekea, ichukue mradi mzima
kama ni ujenzi wa darasa mpaka unakamilika kwa manufaa ya jamii.

“Nafikiria Benki inaweza sasa ikabadiri muelekeo wake kuhusu misaada
mbalimbali kwa jamii, kwa kuhakikisha wanachukua mradi hata mmoja mkubwa
kwenye wilaya na kuhakikisha wanaukamilisha kwa usimamizi wao ambao utaleta
ile thamani halisi ya fedha wanazotoa.” Alisema.

Mjumbe wa Kamatiu Tendaji ya ALAT na Meya wa SUmbawanga – Justine
Malisawa aliishukuru Benki ya NMB kwa kuleta mfumo wa ukusanyaji mapato ya
halmashauri kielektroniki na kuisifia kuwa imeleta mafanikio makubwa kwa
mapato ya Serikali kuongezeka tofauti na ilivyokuwa zamani hasa ndani ya miaka
hii mitatu.

Maneno ya Bwana Malisawa yaliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu wa
Kisarawe na Mjumbe wa Kamati tendaji ya ALAT – Mh Zaynab Vuli huku akisema
Benki hiyo imejipambanua kwa kufika maeneo ambayo Benki zingine hazijafika.

Mh Vulu aliiomba Benki hiyo kupunguza riba na kutoa mikopo nafuu kwa wafanya
biashara wadogo hasa wale wanaofanya biashara zao vijijini ili kusaidia
maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini.