***************
NA EMMANUEL MBATILO.
Wanafunzi watarajiwa watakiwa kuchagua vyuo vilivyobora kwa maendeleo ya elimu hasa katika masuala ya mazingira mazuri yenye utulivu wa kutosha ili kumuwezesha kupata elimu iliyobora kulingana na anavyohitaji.
Ameyasema hayo leo Mkufunzi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).Bw.Omar Kassim katika Maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe Blog, Bw. Omar amewataka wanafunzi watarajiwa waweze kujitokeza katika Chuo hicho kwani wana fani nyingi na fursa katika chuo hicho kwani kimekuwa na ushirikiano mkubwa kati ya Chuo hicho na nchi mbalimbali kama vile Afrika Kusini, Malawi,Kenya,Rwanda,Burundi, Comoros,Botswana pamoja na nchi nyingine za jirani.
Kama ilivyo malengo ya chuo hicho kuwafikia wadau mbalimbali hapa nchini hivyo wameweza kusajili wanafunzi wengi kutoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambao wamejiunga na chuo hicho kwaajili ya masomo hivyo bado wanaendelea kupokea wanafunzi watarajiwa katika nyanja za certificate, diploma na degree pia wanasajili wanafunzi wa Masters na PHD.
“Uwepo wa maonesho ya TCU kwetu sisi ni mlango mkubwa unaotupeleka kwa wadau wengi watanzania na nje ya Tanzania ambao wanakuja hapa tunapata fursa ya ana kwa ana kujadiliana nao na kueleza vision yetu na watu wengi wanakuja hapa kutaka kujiunga na chuo hichi ni mbadala wa elimu kwa Tanzania kwani kimesomesha wataalamu wengi wa nchi hii ambao wamechukua nyadhifa tofauti katika serikali ya Tanzania,Malawi, Zambia, Rwanda na Burundi na kwingineko”. Amesema Bw. Omar.