**************
Na Magreth Kinabo
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema Mahakama ya Tanzania iko tayari kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Upatanishi ‘International Chamber of Commerce’ (ICC) ili kuwezesha Mahakama kusikiliza migogoro kwa njia ya mfumo wa upatanishi( Abitration).
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu, ofisini kwake jijini Dar es Salaam ,wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe watu watano kutoka taasisi hiyo, uliongozwa na Makamu wa Rais wa taasisi hiyo, Profesa . Dkt. Mohamed Wahab.
Awali Makamu huyo wa taasisi hiyo alisema wamefika hapa nchini ili kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu, Profesa Juma kushirikiana Mahakama ya Tanzania kuiwezesha kusikiliza migogoro kwa njia ya mfumo wa upatanishi.
Profesa, Dkt. Wahab aliongeza kwamba tayari nchi nyingine zimeruhusu Mahakama, imeruhusu mfumo huo kutumika na umeonyesha kufanikiwa, ambapo alitolewa mfano nchi ya Afrika Kusini na Mauritania, hivyo wangependa kuona na Tanzania inatumia mfumo huo na taasisi hiyo itatoa mafunzo kwa majaji.
“Ni tunaiomba Tanzania kutengeneza kanuni ili kuwezesha mfumo huo wa upatanishi kuweza kufanya kazi katika Mahakama za Tanzania.
Jaji Mkuu alisema yuko tayari kuwezesha mfumo huo kuanza kutumika nchini kwa kuwa ni muhimu na utawezesha migororo kusikilizwa haraka.
“Tuna sheria ya Upatanishi, ni sheria ya zamani hivyo kuna haja ya kuihuisha ili iendane na mahitaji ya sasa,” alisema Profesa Juma.
Alisema Mahakama inatumia njia ya upatanishi ndani ya kesi za madai, lakini haujaweza kufanya kazi vizuri kwa sababu ya kutoeleweka ipasavyo miongoni mwa wadaawa.
Hivyo aliongeza kwamba ni vizuri majaji na mawakili wakapatiwa mafunzo juu ya masuala hayo.
Profesa Juma aliutaka ujumbe huo kuandaa andiko na kuhusu mfumo huo na kuonyesha mapendekezo yao.
Ujumbe huo umekuwepo nchini tangu Julai 17 na Julai 19 , mwaka huu na umefanya mazungumza na ujumbe wa Tanzania kuhusu masuala ya upatanishi ndani nan je ya, ikiwemo Siku ya Upatanishi iliyofanyika kwenye hoteli ya Slipway, Dar es Salaam Julai 18,mwaka huu na utakuja tena mwakani.