Home Mchanganyiko CHUO CHA KIUT KIMERUHUSIWA KUENDELEA KUDAHILI WANAFUNZI

CHUO CHA KIUT KIMERUHUSIWA KUENDELEA KUDAHILI WANAFUNZI

0

Baadhi ya wanafunzi watarajiwa wakipata huduma katika banda la Chuo Cha KIUT katika Maonesho ya Vyuo vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Kaimu makamu wa Chuo cha KIUT,Ass. Prof.Abanis Turyahebwa akiwa ametembelea banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

**************

NA EMMANUEL MBATILO

Baada ya kustishwa kudahili kwa miaka miwili, Chuo Kikuu cha Kampala nchini Tanzania (KIUT) sasa kimeweza kuruhusiwa kudahili kwa baadhi ya programu zinazopatikana katika Chuo hicho.

Ameyasema hayo leo Mkuu wa Masoko wa Chuo hicho Bw.Neil Mboma katika Maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Fullshangwe blog Bw.Mboma amesema kuwa licha yakuwa walifungiwa kudahiri wanafunzi na Mamlaka ya TCU walikuwa wanaendelea na mafunzo kwa wanafunzi mpaka hadi sasa walivyoruhusiwa kudahili kwa program ishirini na tano (25) na kozi hizo ni zote za biashara, sheria, kompyuta na Social Sciences katika ngazi za certificate, diploma na degree.

“Kwa ushirikiano tunasubiri mamlaka husika kutupa kibali kudahili kozi zilizobaki na udahili unakuwa na msimu kadhaa hivyo tunategemea program hizi kuachiwa”. Bw.Mboma.

Aidha, Bw.Mboma amesema kuwa utaratibu wa kujunga na chuo hicho kwa mwaka huu udahili wote utakuwa unafanyika mtandaoni bure. Hivyo fomu hazitouzwa na amewaomba wanafunzi wasikubali kuuziwa fomu kwaajili ya  kujiunga na chuo hicho.

Pamoja na hayo Bw.Mboma amewataka wanafunzi watarajiwa waweze kufika Chuoni au kutembelea tovuti yao kuweza kujiunga na chuo hicho.