Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa mpango maalumu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Viktoria. Mpango huo ulibainishwa wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa ‘HIGH impact Weather lAke sYstem (HIGHWAY)’ uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Ubungo Plaza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a .
‘Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kuongeza ufanisi wa uandaaji na usambazaji kwa wakati wa taarifa za hali ya hewa hususani taarifa za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Viktoria’, alibainisha Dkt. Chang’a.

