Mkurugenzi ya mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devota Mdachi (Kushoto) akizungumza na ndugu Qui Yu (katikati) ambaye ni Mtendaji wa kampuni ya Tibet Dexin International Financial Leasing Co. Ltd (TDIFL) ya China na Bi Xiao Xinzhu (Kulia) katibu wa TDIFL punde walipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Julai, 2019. Haya ni matunda ya msafara wa kutangaza vivutio vya utalii uliyofanywa na TTB nchini China mwezi Novemba 2018.
Kampuni ya TDIFL inayomilikiwa na Serikali ya jimbo la Sichuan nchini china imeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya utalii na usafiri wa anga ambapo inatarajia kujenga hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota Tano (5) katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro na Karatu ambazo zitakazo gharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 100. Aidha, kwa upande wa usafiri wa anga, TDIFL inatarajia kushirikiana na Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Tanzania (Dar es Salaam/Kilimanjaro) kwenda kwenye mji wa Chengdu uliyopo katika jimbo la Sichuan la nchini China.