Thami Mseleku Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akizungumza katatika wiki ya ufunguzi wa wiki ya Nelson Mandela inayoendelea katika Chuo hicho kilichopo Jijini Arusha.
Washiriki wa Maadhimisho Wiki ya Nelson Mandela inayofanyika katika Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela Jijini Arusha.
Na Vero Ignatus,Arusha
Jamii ya Watanzania imetakiwa kuwawezesha watoto wa kike katika masuala ya sayansi Teknolojia ili waweze kuchochea maendeleo katika Bara la Afrika kupitia sayansi na hata kupelekea maendeleo ya viwanda nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Jamii ya Watanzania imetakiwa kuwawezesha watoto wa kike katika masuala ya sayansi Teknolojia ili waweze kuchochea maendeleo katika Bara la Afrika kupitia sayansi na hata kupelekea maendeleo ya viwanda nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Thami Mseleku ni Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania amesema hayo katika ufunguzi wa Wiki ya Nelson Mandela inayofanyika katika Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela kilichopo jijini Arusha ambapo ameitaka jamii kuhamasisha na kujikita zaidi katika masomo ya sayansi ambayo yanachochea ugunduzi na uvumbuzi utakaosaidia maendeleo ya Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.
Profesa Antony Mshandete ni Kaimu Makamu wa Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela amesema kuwa katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa nelson Mandela wanatafakari jinsi ambavyo Ubunifu,Ugunduzi na Uhandisi unachangia kufikia uchumi wa viwanda na kuharakisha maendeleo kwa ujumla.
Linda Mathayo ni mwanafunzi wakike kutoka shule ya Star High Duluti aliyefika katika Wiki ya Mandela amesema kuwa wiki hiyo imewapa hamasa ya kusoma masomo ya sayansi ili waweze kuwa Wahandisi,Marubani na Watafiti na pia kuondoa utamaduni potofu wa kuwa masomo hayo wanayaweza watoto wa kiume peke yao
Dr.Lilian Pasape ni Mhadhiri Mwandamizi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Mandela amesema kuwa katika wiki ya Mandela watakua na mafunzo Maalumu ya kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi pamoja kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaozunguka chuo hicho.
</div